• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 11:48 AM
Lampard ajiondoa kwenye kivumbi cha kuwa kocha mpya wa Norwich City

Lampard ajiondoa kwenye kivumbi cha kuwa kocha mpya wa Norwich City

Na MASHIRIKA

FRANK Lampard amejiondoa katika mbio za kuwa mrithi wa kocha Daniel Farke kambini mwa Norwich City.

Sogora huyo wa zamani wa Uingereza na Chelsea mwenye umri wa miaka 43 alishiriki mazungumzo na Norwich mapema wiki hii kuhusu uwezekano wa kuwa kocha wao mpya. Alikuwa pia akipigiwa upatu wa kuwa mrithi wa kocha Dean Smith aliyetimuliwa na Aston Villa baada ya msururu wa matokeo duni.

Smith kwa sasa yuko kwenye likizo nchini Amerika na alizungumza pia na Norwich kuhusu uwezekano wa kupokezwa mikoba ya kikosi hicho kabla ya kuondoka Uingereza. Kocha huyo wa zamani wa Brentford alipigwa kalamu na Villa mnamo Novemba 7, 2021 baada ya waajiri wake kupoteza mechi tano mfululizo na hivyo kushuka kwenye msimamo wa jedwali la EPL hadi nafasi ya 16.

Lampard amekuwa nje ya ulingo wa ukocha tangu kipindi chake cha miezi 18 cha kuhudumu kambini mwa Chelsea akiwa kocha kitamatishwe ghafla ugani Stamford Bridge mnamo Januari 2021. Kufikia sasa, Norwich wanavuta mkia kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama tano kutokana na mechi 11 zilizopita.

Mchuano wao ujao utakuwa dhidi ya Southampton mnamo Novemba 20, 2021. Farke alifurushwa na Norwich mnamo Novemba 6, 2021 licha ya kuongoza kikosi hicho kusajili ushindi wa kwanza msimu huu wa 2021-22 baada ya kupepeta Brentford.

Mikoba ya kikosi hicho kwa sasa inashikiliwa na Steve Weaver ambaye ni mkuu wa kitengo cha makuzi ya soka ugani Villa Park. Katika msimu wake wa kwanza ugani Stamford Bridge, Lampard aliongoza Chelsea kuambulia nafasi ya nne kwenye EPL na kutinga fainali ya Kombe la FA.

Ushindi wa 3-1 aliongoza Chelsea kusajili dhidi ya Leeds United mwanzoni mwa Disemba 2020 ulisaidia kikosi hicho kutua kileleni mwa jedwali la EPL kabla ya msururu wa matokeo duni kuteremsha miamba hao hadi nafasi ya tisa mwezi uliofuata. Kabla ya kutua Chelsea, Lampard alikuwa kocha wa Derby County na akaongoza kikosi hicho kutinga fainali ya mchujo wa kupanda ngazi hadi EPL ambapo walizidiwa maarifa na Aston Villa

You can share this post!

Mwendwa apigwa teke

Vijana wengi kuwania 2022 viti vyeo 2022

T L