• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 5:55 PM
Mwendwa apigwa teke

Mwendwa apigwa teke

Sintofahamu imegubika kandanda nchini baada ya Serikali jana kuvunjilia mbali Shirikisho la Soka Nchini (FKF).

Kenya imejitia katika hatari ya kupigwa marufuku na Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa) kushiriki katika mechi za kimataifa kufuatia hatua hiyo.Serikali kupitia kwa Waziri wake wa Michezo Amina Mohamed ilichukua hatua hiyo jana na kuteua kamati ya muda ya watu 15 kusimamia shughuli za kandanda nchini kwa miezi sita baada ya kugunduliwa namna ufisadi ulivyokithiri FKF tangu Nick Mwendwa achukue usukani miaka sita iliyopita.

“Naitarajia Fifa kutusaidia kuzima ufisadi mpirani, badala ya kutupiga marufuku,” alisema Amina baada ya kupokea ripoti ya uchunguzi kutoka kwa Msajili wa Vyama vya Umma, Rose Wasike.Kamati mpya inayoongozwa na Jaji mstaafu Aaron Ringera, huku wengine wakiwa Generali mstaafu Moses Oyugi, Fatma Adan, Philip Musyimi Mue,

Anthony L. Isayi, Elisha Chepchieng Kiplagat, Hassan Mahmoud Haji, Fredrick Tureisa Lekesike, Mwangi Muthee, Neddy Atieno Okoth, Ali Amour, Titus Kasuve, Richard Omwela, Bobby Ogolla na JJ Masiga.

Uchunguzi ulioendeshwa na DCI ulitaka kujua jinsi Sh244.6m za kuandaa Harambee Stars kabla ya fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon) mnamo 2019 zilivyotumika, pamoja na Sh11 milioni na pia Sh57m zilizotengwa kugharamia marupurupu ya wachezaji wa timu hiyo ya taifa.

Imedaiwa kwamba afisi ya Mwendwa imetumia vibaya Sh2.5 bilioni kati ya mwezi Juni 2019 na Disemba 2019. Kadhalika Serikali inataka kuelezwa jinsi Sh11 milioni zilitolewa kwa akaunti ya FKF na kutumwa kwa akaunti binafsi ya Nick Mwendwa.Kwa mfano, imegunduliwa maafisa wakuu Anthony Makau, Charles Ouma,

Murithi Nabea na Doris Petra walipokea Sh500,000 kila mmoija na huenda pamoja na Mwendwa wakafunguliwa mashtaka ya ufisadi.Katika hali hiyo ya kushangaza, mwanakamati Chris Amimo alipokea Sh6.5m mnamo Septemba 27, 2019 na baadaye Sh950,000 siku hiyo. Mwanakamati mwingine kutoka jimbo la Magharibi alipata Sh2m zimetumwa kwa akaunti yake.

Imegunduliwa kwamba pesa hizo zilikuwa zikitumwa moja kwa moja kutoka kwa akaunti ya Mwendwa ya Kenya Commercial Bank, ilhali hawajapangiwa mshahara wowote.Mnamo Novemba 2019 FKF ilitengeneza ripoti ya matumizi yake ya kifedha, lakini Wizara ya Michezo haikuridhika na ripoti hiyo na ikabidi iwasilishe ripoti hiyo kwa Mugakuzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Nancy Gathungu aliyedai Mwendwa hakueleza alichofanyia Sh11 milioni.

Mwendwa alichukua uongozi kutoka kwa Sam Nyamweya mnamo Februari 2016, lakini tangu wakati huo Wakenya wameshuhudia wadhamini wakikatiza mikataba na afisi ya Mwendwa ambaye pia hajaeleza jinsi Sh135m za gari maalum la OB zilikoenda.Kadhalika Mwendwa amechunguzwa kuhusu pesa za wadhamini Startimes na BetKing.

Kila timu KPL ilifaa kupokea Sh8mambapo kila timu ya ligi kuu ilitarajiwa kupokea Sh8 milioni kila msimu hadi 2025.Hatua ya Serikali imetokea wakati Harambee Stars inashiriki katika mechi za mchujo wa kufuzu kwa Kombe la Dunia, huku Vihiga Queens ikiwakilisha taifa katika mashindano ya Klabu Bingwa barani Afrika.

You can share this post!

Villa yamwaga 674 Millioni kunyakua kocha Gerald

Lampard ajiondoa kwenye kivumbi cha kuwa kocha mpya wa...

T L