• Nairobi
  • Last Updated May 5th, 2024 8:50 AM
Leicester City kupimana ubabe na Napoli katika Europa League

Leicester City kupimana ubabe na Napoli katika Europa League

Na MASHIRIKA

LEICESTER City watamenyana na Napoli, Spartak Moscow na Legia Warsaw katika Kundi C la kampeni za Europa League msimu huu wa 2021-22.

Kwa upande wao, West Ham United watapepetana na Dinamo Zagreb, Genk na Rapid Vienna katika Kundi H.

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Scotland, Rangers wametiwa katika Kundi A kwa pamoja na Olympique Lyon, Sparta Prague na Brondby.

Celtic ambao pia ni miamba wa soka nchini Scotland, wametiwa katika Kundi G linalojumuisha pia Bayer Leverkusen, Real Betis na Ferencvaros.

Katika kipute kipya cha Europa Conference League, Tottenham watamenyana na Rennes, Vitesse na NS Mura ya Slovenia katika Kundi G.

Mechi za mkondo wa kwanza za hatua ya makundi zimeratibiwa kusakatwa mnamo Alhamisi ya Septemba 16, 2021 huku zile za raundi ya mwisho zikipangwa kutandazwa mnamo Disemba 9, 2021.

Kwa mujibu wa waratibu wa vipute vya Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa), fainali ya Europa League msimu huu itachezewa uwanjani Ramon Sanchez Pizjuan jijini Seville, Uhispania mnamo Jumatano ya Mei 18, 2021.

Fainali ya makala ya kwanza ya Europa Conference League itachezewa katika uwanja wa Air Albania jijini Tirana mnamo Jumatano ya Mei 25, 2021.

Chini ya kocha Brendan Rodgers, Leicester walikamilisha kampeni za EPL katika nafasi ya tano mnamo 2020-21 na kufuzu kwa kipute cha Europa League kwa mwaka wa pili mfululizo. Kwa upande wao, West Ham walifunga kampeni hizo za EPL katika nafasi ya sita na kujikatia tiketi ya kushiriki Europa League kwa mara ya kwanza katika historia.

Leicester walitinga hatua ya 32-bora kwenye Europa League mnamo 2020-21 na wakadenguliwa na Slavia Prague kwa jumla ya mabao 2-0.

Kabla ya droo ya Europa League na Europa Conference League kufanyika, fowadi wa Villarreal, Gerard Moreno alitawazwa Mchezaji Bora wa Europa League katika msimu wa 2020-21 baada ya kuwapiku wanasoka wawili wa Manchester United – Bruno Fernandes na Edinson Cavani.

DROO YA EUROPA LEAGUE:

KUNDI A: Lyon, Rangers, Sparta Prague, Brondby.

KUNDI B: Monaco, PSV Eindhoven, Real Sociedad, Sturm Graz.

KUNDI C: Napoli, Leicester, Spartak Moscow, Legia Warsaw.

KUNDI D: Olympiakos, Eintracht Frankfurt, Fenerbahce, Royal Antwerp.

KUNDI E: Lazio, Lokomotiv Moscow, Marseille, Galatasaray.

KUNDI F: Braga, Red Star Belgrade, Ludogorets, Midtjylland.

KUNDI G: Bayer Leverkusen, Celtic, Real Betis, Ferencvaros.

KUNDI H: Dinamo Zagreb, Genk, West Ham, Rapid Vienna.

DROO YA EUROPA CONFERENCE LEAGUE:

KUNDI A: LASK, Maccabi Tel-Aviv, Alashkert, HJK Helsinki.

KUNDI B: Gent, Partizan, Flora Tallinn, Anorthosis Famagusta.

KUNDI C: Roma, Zorya Luhansk, CSKA Sofia, Bodo/Glimt.

KUNDI D: AZ Alkmaar, CFR Cluj, Jablonec, Randers.

KUNDI E: Slavia Prague, Feyenoord, Union Berlin, Maccabi Haifa.

KUNDI F: FC Copenhagen, PAOK, Slovan Bratislava, Lincoln Red Imps.

KUNDI G: Tottenham, Rennes, Vitesse, NS Mura.

KUNDI H: Basel, Qarabag, Kairat Almaty, Omonoia.

You can share this post!

Vita vya kujipima nguvu ugavana Kiambu vyaanza

MUTUA: Afrika yafaa ijitengenezee chanjo, iache kulalamika