• Nairobi
  • Last Updated May 14th, 2024 8:55 AM
Liverpool wakomoa Aston Villa na kuendeleza presha kwa Man-City kileleni mwa jedwali la EPL

Liverpool wakomoa Aston Villa na kuendeleza presha kwa Man-City kileleni mwa jedwali la EPL

Na MASHIRIKA

LIVERPOOL walitoka nyuma na kupepeta Aston Villa 2-1 mnamo Jumanne usiku ugani Villa Park katika ushindi ulioendeleza presha kwa viongozi na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), Manchester City.

Chini ya kocha Jurgen Klopp, Liverpool walijikuta chini kunako dakika ya taty baada ya Villa kuwekwa kifua mbele na Douglas Luiz. Hata hivyo, mabingwa hao mara 19 wa EPL walirejea mchezoni katika dakika ya sita kupitia bao la Joel Matip kabla ya Sadio Mane kujaza kimiani krosi ya Luis Diaz katika dakika ya 65.

Ushindi wa Liverpool wanaofukuzia mataji matatu zaidi msimu huu, yakiwemo ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) na Kombe la FA, uliwasaza katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa jedwali la EPL kwa alama 86 sawa na Man-City ambao wana mechi moja zaidi ya kusakata ili kufikia idadi ya michuano 36 ambayo imetandazwa na Liverpool.

Fowadi wa zamani wa Liverpool, Danny Ings alipoteza nafasi nyingi za kusawazishia Villa katika kipindi cha pili huku pigo la pekee kwa Liverpool likiwa ni jeraha la mguu ambalo huenda likamweka nje kiungo mkabaji Fabinho wakati wa fainali ya Kombe la FA itakayokutanisha waajiri wake na Chelsea mnamo Mei 14, 2022 ugani Wembley.

Tofauti na Liverpool ambao walikuwa na kibarua kizito cha kujinyanyua baada ya Tottenham Hotspur kuwalazimishia sare ya 1-1 ugani Anfield katika mechi ya awali ya EPL, Villa walikuwa na kiu ya kuendeleza ubabe uliowavunia ushindi dhidi ya Norwich City (2-0) na Burnley (3-1) katika mechi mbili za awali.

Villa sasa wamejizolea alama saba kutokana na mechi nne zilizopita za EPL huku wakifungwa mabao matatu. Matokeo hayo yamewaweka katika nafasi ya 11 jedwalini kwa alama 43 sawa na Brentford na Newcastle United.

Baada ya kuvaana na Chelsea kwenye fainali ya Kombe la FA mnamo Mei 14, 2022 ugani Wembley, Liverpool watatoanajasho na Real Madrid ya Uhispania kwenye fainali ya UEFA itakayochezewa jijini Paris, Ufaransa mnamo Mei 28, 2022.

Tofauti na Man-City ambao wametikisa nyavu za wapinzani wao mara 89 na kufungwa mabao 21, Liverpool wamepchika wavuni magoli 89 na kuokota mpira kimiani mara 24.

Liverpool sasa wameshinda mechi nne mfululizo dhidi ya Villa katika mashindano yote tangu wapokeze kikosi hicho kichapo cha 7-2 katika EPL ugani Villa Park mnamo Oktoba 2020.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wanasheria washauri wabunge waondoe makali ya kuumiza raia...

Matiang’i ashutumu sheria kwa kuruhusu washukiwa kuwania

T L