• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 7:55 PM
Matiang’i ashutumu sheria kwa kuruhusu washukiwa kuwania

Matiang’i ashutumu sheria kwa kuruhusu washukiwa kuwania

Dkt Matiang’i alisema kuwa sheria hizo hafifu zinawezesha wanasiasa kutumia mabilioni ya hela za wizi katika kampeni bila wahusika kuulizwa walipozitoa.

Waziri Matiang’i aliondolea lawama Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kuhusu wanasiasa kutumia mabilioni ya fedha katika kampeni zao.

“Sheria zilizopo kuhusu usimamizi wa fedha ni hafifu. Hivyo kuna hatari kwamba asilimia 40 ya viongozi watakaochaguliwa watakuwa wahalifu,” akasema.

Dkt Matiang’i alikuwa akizungumza mjini Naivasha, Kaunti ya Nakuru wakati wa kongamano la kitaifa la kujadili mageuzi katika mfumo wa upatikanaji haki.

Kuna wanasiasa kadhaa ambao wamepewe tiketi na vyama mbalimbali kuwania vyeo vya kisiasa kwenye uchaguzi ujao licha ya kuwa na kesi hasa kuhusu ufisadi na hata mauaji.

IEBC imesema kuwa kisheria haina uwezo wa kuzima washukiwa hao, hivyo ni juu ya Wakenya kuamua iwapo watawachagua.

Wengine waliohudhuria kongamano hilo ni Jaji Mkuu Martha Koome, Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati, Mkuu wa Mashtaka ya Umma Noordin Haji na Mkurugenzi wa Idara ya Kuchunguza Uhalifu (DCI) George Kinoti.

Katika mkutano huo, Waziri Matiang’i pia alisema kuwa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yanahatarisha usalama na amani nchini huku uchaguzi ukikaribia.

  • Tags

You can share this post!

Liverpool wakomoa Aston Villa na kuendeleza presha kwa...

TAHARIRI: Uadilifu ndiyo chanjo ya siasa chafu za Kenya

T L