• Nairobi
  • Last Updated April 27th, 2024 3:16 PM
Malkia wa 1,500m alivyoanza kung’aa

Malkia wa 1,500m alivyoanza kung’aa

Na BERNARD ROTICH

BINGWA mara mbili wa mbio za Olimpiki katika mita 1,500 Faith Kipyegon Chepng’etich, anajiandaa kwa kibarua cha kuwania taji la Riadha za Dunia zitakazofanyika mjini Eugene, Marekani mnamo Julai 2022.

Vilevile, Chepng’etich amekuwa akifanya mazoezi mjini Kaptagat, Kaunti ya Elgeyo Marakwet, kwa minajili ya msimu mpya wa riadha za msururu wa IAAF Diamond League pamoja na mashindano ya Jumuiya ya Madola nchini Uingereza mwezi Agosti 2022 .

Ni zaidi ya mwongo mmoja sasa tangu atue katika jukwaa la mabingwa.Nyota yake ilianza kung’aa aliposhiriki mbio zake za kwanza zilizokuwa za Nyika, katika mashindano ya dunia mjini Bydgoszcz, Poland, mwaka 2010.Alimaliza katika nafasi ya nne kitengo cha akinadada chipukizi, ambacho huwa ni mbio za kilomita sita.

Mwaka uliofuatia, alikuwa ameshapata uzoefu na aliibuka kidedea katika mashindano yayo hayo ya Nyika kwa akinadada chipukizi, akiandikisha muda wa dakika 18:53 mjini Punta Umbria, Uhispania.Ni hapo alijipatia medali yake ya kwanza kabisa ya dhahabu, na pia ya kwanza katika mbio za Nyika.

Mwaka huo alijumuishwa katika kikosi cha mashindano ya Riadha za Vijana Ulimwenguni mjini Lille, Ufaransa.Alishiriki kitengo cha 1,500m kwa mara ya kwanza kabisa na kujinyakulia medali ya dhahabu; ya pili katika kabati lake la makombe, na ya kwanza kabisa katika mbio za uwanjani.

Ni mahali hapa ndipo alitambua uwezo alionao kuteka mbio hizo za mizunguko nne, akaamua kuzamia kwa mazoezi kabambe.Mwaka 2012 aliunga kikosi kilichoelekea Barcelona nchini Uhispania kushiriki Riadha za Vijana.Akaibuka tena mshindi katika mbio za 1,500m.

Hata hivyo, mwaka huo alimaliza nambari 21 katika Michezo ya Olimpiki jijini London, Uingereza.“Sikuwa nimepata uzoefu kamili wakati huo, lakini ilikuwa funzo muhimu sana kwani nilijinoa sawasawa,” Chepng’etich aliambia Dimba.

Tangu wakati huo, amejiongezea dhahabu katika Mbio za Nyika Duniani 2013 mjini Bydgoszcz, Poland; Michezo ya Jumuiya ya Madola 2014 mjini Glasgow, Uingereza; Olimpiki za Rio 2016 nchini Brazil; Riadha za Dunia 2017 jijini London; na Olimpiki za Tokyo 2020 nchini Japan alikotetea taji lake.

Chepng’etich ananolewa na makocha wawili; Patrick Sang na Richard Metto, ambao anasema wamekuwa msaada mkubwa kwake.Mwaka wa 2013 aliweza kushinda mbio za nyika duniani kule Bydgoszcz, Poland kitengo cha vijana kabla ya kuibuka kwenye nafasi ya tano kwenye mbio za dunia kule Moscow, Urusi katika mbio za mita 1,500.

Aliwakilisha nchi kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola kule Glasgow, Uingereza mwaka wa 2014 mahali alijipatia dhahabu kabla ya kushiriki Mbio za Dunia kule Beijing, Japan mahali aliibuka wa pili.Alielekea Rio de Janeiro Brazil mahali aliweza kuibuka mshindi kwenye mbio hizo za mita 1,500 kabla ya kunyakua dhahabu kwenye Mbio za Dunia kule London, Uingereza mwaka wa 2017.

Alielekea likizo mwaka huo kujifungua mwana wake wa kawanza na 2019 alijibwaga uwanjani tena mahali aliweza kujishindia medali ya fedha kwenye mbio za mita 1,500.Katika Mbio za Almasi kule Florence Italia alipoanza msimu wake, Chepngetich alitimka na mpinzani wake mkuu Sifan Hassan kutoka Uholanzi mahali aliibuka wa pili nyuma ya Sifan.

Alidokeza kuwa anapenda sana kutimka na Sifan kwa sababu ya upinzani ambayo yuko nayo lakini anatarjia kufanya vyema ifikapo mashindano ya Olimpiki.Mwanariadha huyo yuko na kocha wawili Patrick Sang na Richard Metto ambao anasema wamekuwa wa msaada kwake.

Mwanariadha huyo amaekuwa akifanya mazoezi na watimkaji kama vile mshikilizi wa rekodi kwenye mbio za marathon Eliud Kipchoge, aliyekuwa bingwa wa mbio za nusu marathon Geoffrey Kamworor ikiwemo wengine.

Akiongea na Dimba, Chepngetich alisema kuwa alifurahia msimu uliopita na yuko na raha kwa sababu aliweza kushiriki mbio za Olimpiki baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kwa sababu ya homa ya korona na kutetea taji lake kwa mara ya pili.

“Raha yangu ni kuwakilishi nchi ya Kenya kimataifa na baada ya kuongoza kwenye majaribio ya mbio kule Kasarani, Nairobi, niliweza kuelekea Tokyo mahali nilitetea taji langu hata baada ya kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Mholanzi Sifan Hassan” akaeleza kidosho huyo ambaye ni mshikilizi wa fedha kwenye mbio za dunia.

Chepngetich alianza msimu wake kwa kushiriki Mbio za Almasi mkondo wa Doha mahali alishiriki kwenye mbio za mita 800 na akaibuka mshindi alipoandikisha muda wa 1:58.26.“Nilishiriki mbio za mita 800 ili niweze kuongeza kasi yangu kama njia moja ya kujitayarisha kwenye mbio za mita 1,500 kule Japan kwenye mashindano ya Olimpiki na nilikuwa ninataka kuongeza kasi haswa kwenye mita 100 ya mwisho,” akasema Chepngetich.

Mwanaspoti huyo ambaye amesajiliwa na Global Sports Communication kutoka Uholanzi yuko kwenye kambi moja na Geoffrey Kamworor (10,000), Rodgers Kwemoi (10,000), Hyvine Kiyeng (3,000) ambaye atawakilisha kwenye mbio za mita 3,000 kuruka viunzi na maji miongoni mwa wengine.

You can share this post!

Kylian Mbappe anayeaminiwa na Paris Saint-Germain na...

Ari ya kisasi ilimsukuma kwa ndondi

T L