• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 8:50 AM
Ari ya kisasi ilimsukuma kwa ndondi

Ari ya kisasi ilimsukuma kwa ndondi

Na GEOFFREY ANENE

SARAH Achieng’ Ndisi hakudhania atafanikiwa kuwa bondia mtajika baada ya mazoezi yake ya kwanza mapema 2008, katika ukumbi wa Kariobangi North jijini Nairobi.

Hata hivyo, Achieng’ (pichani)sasa ni malkia mpya wa masumbwi akifuata nyayo za Conjestina Achieng’ na Fatuma Zarika.Hii ni baada yake kumpangua Anisha Basheel kutoka Malawi katika pigano la taji ya Jumuiya ya Madola la uzani wa kati ya kilo 61.2 na kilo 63.5 (Super Lightweight).

Mchapano huo ulifanyika ukumbi wa Charter Hall, Nairobi, mwezi jana Oktoba 20. Achieng’, 34, anafahamika kwa jina la utani kama Angel of War, alilopewa na kocha wake Alfred Analo Anjere maarufu kama Coach Priest.

Kilichomchochea azamie ubondia ni kusudi la kulipiza kisasi. Alizabwa kofi na mwanamume aliyetoka nyuma na kuchomoka bila kuonyesha uso wake.“Sikuamini nitafaulu katika ndondi sababu nilipenda kususia mazoezi. Lakini, tangu kisa hicho nilipata motisha kamili wa kuwa bondia ili niwafunze adabu wanaume wengine mwenye tabia chwara kama hiyo,” alieleza Dimba katika mahojiano.

Achieng’ – ambaye mume wake James Onyango Omogo ni bingwa wa zamani wa dunia taji la WBF uzani wa Welter – alipata Sh4,000 kutoka pigano lake la kwanza alilopoteza dhidi ya Mkenya Bena Kaloki mnamo Agosti 9, 2008. Hakufa moyo.

Alianza kuona matunda yake 2010 aliposhinda mapigano manane mfululizo. Mnamo 2015 alibeba taji la kimataifa la UBO InterContinental uzani wa Lightweight.Anajivunia rekodi ya kushinda michapano 14 – akiwa ameshinda mapambano sita mfululizo – na kupoteza mara mbili pekee.

Ushindi dhidi ya Basheel ulimzolea fedha zisizopungua laki moja. akimduwaza mwenyeji Marina Popova wa Urusi Desemba 5.Anajivunia rekodi ya kushinda michapano 14 – akiwa ameshinda mapambano sita mfululizo – na kupoteza mara mbili pekee.

Ushindi dhidi ya Basheel ulimzolea fedha zisizopungua laki moja. kabla ya Mkenya Judy Waguthii kumpiga breki mwezi Desemba 2014.Malkia huyu alipata mafanikio makubwa mnamo 2015 ikiwemo taji la kimataifa la UBO InterContinental uzani mwepesi, baada ya kuduwaza mwenyeji Marina Popova nchini Urusi mnamo Desemba 5.

Anajivunia rekodi ya kushinda michapano 14 – akiwa ameshinda mapambano sita mfululizo – na kupoteza mara mbili pekee. Ushindi dhidi ya Basheel ulimzolea fedha zisizopungua laki moja.

You can share this post!

Malkia wa 1,500m alivyoanza kung’aa

Hii ndoto ya dereva chipukizi Yuvraj

T L