• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:55 AM
Man-United tayari kuweka mezani Sh13 bilioni kwa ajili ya maarifa ya fowadi Harry Kane

Man-United tayari kuweka mezani Sh13 bilioni kwa ajili ya maarifa ya fowadi Harry Kane

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United wako radhi kuweka mezani kima cha Sh13 bilioni kwa ajili ya kumshawishi fowadi na nahodha wa Tottenham Hotspur, Harry Kane, 27, kutua ugani Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

Hata hivyo, gazeti la The Sun limesisitiza kwamba hatua hiyo ya Man-United imechochewa na msukumo wa kutaka kutuliza mashabiki wao walioandamana mnamo Mei 2, 2021 nje ya uwanja wa Old Trafford na kusababisha mchuano wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) uliokuwa ukutanishe Man-United na Liverpool kuahirishwa.

Zaidi ya mashabiki 200 wa Man-United waliozua vurugu, kuharibu mali na kujeruhi maafisa wawili wa usalama, walikuwa wakilalamikia hatua ya familia ya Glazer ambao ni wamiliki wa kikosi hicho kutia Man-United kwenye kipute kipya cha European Super League.

Ingawa Spurs hawako radhi kumtia Kane mnadani, kocha Ole Gunnar Solskjaer amesisitiza kwamba ujio wa sogora huyo raia wa Uingereza utaimarisha zaidi safu yake ya uvamizi na kuwezesha kikosi chake hicho kuinua viwango vya ushindani kati yao na wapinzani wao wakuu jijini Manchester – Manchester City ambao wanahitaji alama tatu pekee kutokana na mechi nne zilizosalia ili kutwaa ufalme wa EPL muhula huu.

Kwa upande wake, Kane ambaye amefungia Spurs jumla ya mabao 31 na kuchangia mengine 16 katika mapambano yote ya msimu huu, amesema kwamba kubwa zaidi katika maazimio yake ni kuchezea kikosi kitakachompa fursa ya kuanza kujivunia mataji.

Katika jaribio la kuwavunja moyo Man-United, mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy, amesisitiza kwamba klabu yoyote inayowania maarifa ya Kane mwishoni mwa msimu huu itahitajika kuweka mezani kima cha Sh28 bilioni.

Ingawa Levy ameshikilia kuwa Spurs hawana nia ya kuzinadi huduma za Kane msimu huu, amefichua kwamba muda wa kumtia mnadani sogora huyo utakapowadia, hawatakuwa radhi kumuuza kwa mpinzani wao yeyote katika EPL.

Kane angali na muda wa miaka mitatu katika mkataba mpya wa miaka sita aliotia saini kambini mwa Tottenham mnamo Juni 2018.

Kwa mujibu wa magazeti mengi nchini Uingereza, huenda Tottenham wakawa radhi zaidi kumuuza Kane ili kupunguza gharama ya kumdumisha kimshahara na pia wajipe fedha zitakazowawezesha kujisuka upya.

Ukubwa wa gharama ya kuwadumisha baadhi ya masupastaa wao, ni kati ya sababu zilizowachochea Tottenham pia kuagana na kiungo matata mzawa wa Denmark, Christian Eriksen aliyejiunga na Inter Milan ya Italia mwanzoni mwa mwaka huu.

Sh28 bilioni ni kima cha pesa zilizotumiwa na miamba wa soka ya Ufaransa, Paris Saint-Germain (PSG) kujitwalia huduma za nyota Neymar Jr kutoka Barcelona, Uhispania mnamo 2017.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Kocha Koeman atoa orodha ya wachezaji sita anaotaka...

Mradi wa ujenzi wa Thika Flyover kugharimu Sh3 bilioni