• Nairobi
  • Last Updated May 1st, 2024 10:08 PM
Man-United wamtwaa rasmi beki Raphael Varane kutoka Real Madrid

Man-United wamtwaa rasmi beki Raphael Varane kutoka Real Madrid

Na MASHIRIKA

MANCHESTER United wamekamilisha usajili wa beki Raphael Varane kutoka Real Madrid kwa mkataba wa miaka minne.

Uhamisho wa Varane uligharimu Man-United Sh5.3 bilioni na ada hiyo inakisiwa kufikia Sh6.6 bilioni baada ya mahitaji yote mengine kujumuishwa.

Hadi alipokubali kutua uwanjani Old Trafford mnamo Julai 26, 2021, Varane alikuwa ametwalia Real mataji matatu ya Ligi Kuu ya Uhispania (La Liga) na manne ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) katika kipindi chake cha miaka 10 uwanjani Santiago Bernabeu.

Varane alianza kusakata soka kitaaluma kambini mwa Lens nchini Ufaransa kabla ya kuhamia Real alikowajibishwa mara 360.

Amechezea timu ya taifa ya Ufaransa mara 79 na aliwajibishwa katika michuano yote minne iliyopigwa na taifa hilo kwenye fainali za Euro 2020 kabla ya kubanduliwa kwenye hatua ya 16-bora.

Man-United wamekuwa wakiwania maarifa ya Varane kwa muda mrefu. Baada ya jaribio la kocha Sir Alex Ferguson kumsajili mnamo 2011 kuambulia pakavu, Man-United walijaribu tena kupitia kocha Jose Mourinho mnamo 2017 bila mafanikio.

Varane anakuwa mwanasoka wa tatu kujiunga na Man-United muhula huu baada ya kipa Tom Heaton na Jadon Sancho aliyesajiliwa kwa Sh11.3 kutoka Borussia Dortmund.

Varane anatarajiwa kushirikiana pakubwa na Harry Maguire, Victor Lindelof na Eric Bailly katika safu ya nyuma ya Man-United ambao kwa sasa wanatiwa makali na kocha Ole Gunnar Solskjaer.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Wanavoliboli wa Kenya Prisons wakanyaga DCI ligi ya kina...

Man-United wakomoa Leeds United na kutuma onyo kwa...