• Nairobi
  • Last Updated February 22nd, 2024 1:05 PM
Mashabiki Nakuru kuona Safari Rally angani kwa ndege

Mashabiki Nakuru kuona Safari Rally angani kwa ndege

Na GEOFFREY ANENE

MASHABIKI wa mbio za magari ambao ni wateja wa benki ya KCB watapata fursa ya kipekee ya kushuhudia kivumbi cha Safari Rally kutoka angani katika maeneo ya mashabiki ya Naivasha na Nakuru.

Hii ni baada ya benki hiyo kuzindua helikopta itakayobeba zaidi ya mashabiki 36 watakaoshiriki shindano la benki hiyo litakaloendeshwa kupitia mitandao yake ya kijamii na kwenye tovuti yake.

Shindano hilo lilianza hapo jana. Washindi baada ya droo kufanywa kila siku, watapata fursa ya kuabiri ndege hiyo hadi katika maeneo ya Longonot, Soysambu Farm na Hell’s Gate wakati wa Safari Rally mnamo Juni 24-27.

Akizungumza katika hafla ya kuzindua shindano hilo katika makao makuu ya Safari Rally katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani, kaimu Mkurugenzi wa Mauzo, Mawasiliano na Uraia, Wanyi Mwaura alisema benki hiyo inawapa mashabiki wa mbio za magari fursa ya kufurahia duru hiyo ya sita.

Safari Rally inarejea kwenye ratiba ya dunia (WRC) baada ya miaka 19, huku KCB ikidhamini makala haya kwa Sh100 milioni.Baadhi ya madereva shupavu ambao watapaisha magari yao katika duru ya Safari Rally ni bingwa mtetezi Sebastien Ogier (Ufaransa) pamoja na Muingereza Elfyn Evans kutoka timu ya Toyota na Mbelgiji Thierry Neuville wa timu ya Hyundai.

Ogier anaongoza msimu huu kwa alama 106 kutoka na duru tano za kwanza.

  • Tags

You can share this post!

Mungu hutoa riziki kwa waja wake wanaoomba na kuitafuta kwa...

TAHARIRI: Tumalize uhuni wa wanafunzi shuleni