• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Mashabiki wa Man Utd wafokea nahodha Maguire licha ya klabu kushinda mechi za kujipima nguvu Australia

Mashabiki wa Man Utd wafokea nahodha Maguire licha ya klabu kushinda mechi za kujipima nguvu Australia

Na MASHIRIKA

MELBOUNE, Australia

Nahodha wa Manchester United, Harry Maguire ameendelea kukabiliana na foka za mashabiki, licha ya klabu hiyo kuendelea kufanya vizuri katika mechi za kujipima nguvu nchini Australia.

Kocha mpya wa klabu hiyo, Erik ten Hag amethibitisha Mwingereza huyo mwenye umri wa miaka 29 kama nahodha wa klabu hiyo, siku chache baada ya kusajili Lisandro Martinez kwa Sh5 bilioni, lakini mashabiki hawajaridhika na kiwango chake.

Waandishi wa habari waliokuwa uwanjani kuandika habari za mechi ambayo United waliishinda Crystal Palace 3-1 ugani Melboune Cricket Ground walimuuliza Ten Hag sababu iliyofanya mashabiki kumfokea kocha huyo, lakini alimtetea akisema Maguire alicheza vizuri kwa jumla.

“Ni vigumu kutambua waliomfokea kwa vile uwanja ulikuwa na zaidi ya mashabiki 76,000, lakini hilo halitavuruga mawazo yake. Tutaendelea kujipima nguvu hapa ambapo baada ya mechi ifuatayo mjini Perth Jumamosi na baadaye Oslo mnamo Julai 30,’ akasema.

Kufikia sasa, United wamefunga jumla ya mabao 11 katika mechi tatu za kirafiki, huku Anthony Martial akifunga bao katika kila moja.

Diogo Dalot, Jadon Sancho, Marcus Rashord na kipa David de Gea ni miongoni mwa wachezaji wa United wanaoendelea kuonyesha kiwango cha juu uwanjani kwenye ziara hiyo.

You can share this post!

Uhuru atangaza rasmi kupunguzwa kwa bei ya unga

Hisia mseto Sri Lanka ikipata rais mpya

T L