• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 2:29 PM
Mashabiki wa soka jijini Kisumu wapata utamu wa Kombe la Dunia

Mashabiki wa soka jijini Kisumu wapata utamu wa Kombe la Dunia

NA AREGE RUTH

MASHABIKI wa soka jijini Kisumu, walipata burudani aali siku ya Jumamosi walipotizama mechi za robo-fainali za Kombe la Dunia ambapo Morocco iliinyuka Ureno 1-0 nayo Ufaransa ikachapa Uingereza magoli 2-1.

Mashabiki hao walikusanyika katika eneo la Arina jijini Kisumu na kutizama mechi hiyo kupitia runinga kubwa kwa hisani ya kampuni kubwa ya vinywaji ya Coca-Cola.

Wakazi wa eneo hilo David Kogola na Donald Ochieng walijishindia runinga za skrini za ukubwa wa inchi 32 na 42 mtawalia baada ya kufanya utabiri sawa kwenye mechi hizo.


Shabiki wa soka kutoka katika Kaunti ya Kisumu David Kogola ambaye alijishindia runinga. PICHA | AREGE RUTH

Kogola anasema, “Hii runinga ambayo nimeshinda nitampa mamangu kama zawadi. Huku mashinani pia tukumbukwe kila wakati na sio wakati wa Kombe la Dunia pekee, tunajitaji zawadi kama hizi pia.”

Kwa upande wa mkuu wa mauzo wa Coca Cola Paul Oloo, anasema lengo lao kuu ni kuhakikisha Wakenya kutoka mashinani pia wamepata nafasi ya kuonja utamu wa Kombe la Dunia.

“Tulitenga muda huu kuwapa mashabiki wa soka burudani. Tuna mkataba na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) hivyo tulitaka Wakenya ambao hawakuweza kufika Qatar pia waweze kutizama mechi,” alisema Oloo.

Kando na Kisumu, kaunti za Nairobi, Mombasa na maeneo ya Bonde la Ufa, wakazi wameweza kutizama burudani hiyo. Wakati wa mechi za nusu fainali, kampuni hiyo ya vinywaji itakita kambi kaunti ya Mombasa.

Kombe la Dunia: Mashabiki wa soka kutoka katika Kaunti ya Kisumu wakifuatilia mechi ya awamu ya robo fainali. PICHA | AREGE RUTH

Kampuni hiyo pia ndiyo mshirika wa muda mrefu zaidi na endelevu wa mojawapo ya majukwaa makubwa zaidi ya michezo duniani. Kwa sasa ndio wadhamini wakuu wa Kombe la Dunia nchini Qatar.

  • Tags

You can share this post!

Raila akubali mfupa wa Ruto

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Ufaransa wabandua Uingereza na...

T L