• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Mgomo wanukia ligini EPL

Mgomo wanukia ligini EPL

LONDON, Uingereza

Na MASHIRIKA

Mvutano kati ya Shirikisho la Soka Uingereza (FA) upande mmoja na wachezaji na makocha upande mwingine kuhusu hofu ya kusakata mechi nyingi katika kipindi kidogo huenda ukasababisha mgomo.

Makocha walikutana kivyao pia wachezaji mnamo Alhamisi kuzungumzia mrundiko wa mechi wakati huu wa ongezeko la virusi vya corona. Vyombo vya habari nchini Uingereza vimenukuu kocha wa Manchester City, Pep Guardiola akisema kuwa wachezaji na makocha wawazie kuwa na mgomo kuhusu maslahi ya wachezaji ili viongozi wa soka wawachukulie kwa uzito.

Wakati huu visa vya maambukizi vinaongezeka kwenye Ligi Kuu na kusababisha mechi zaidi ya 10 ziahirishwa, klabu zimeratibiwa kuwa na siku tatu za mechi kila moja kati ya Desemba 26 na Januari 1. Guardiola alipendekeza kuwa wachezaji na makocha wanafaa kugoma ili wapunguziwe mzigo wa mechi nyingi.’

Hatutapata kusikizwa kupitia kupiga domo tu. Kwa viongozi wa Shirikisho la Soka Duniani, Ligi Kuu, vyombo vya habari biashara ni muhimu kuliko maslahi. Kuna ligi zilizokubali kutumia wachezaji watano wa akiba, sisi hapa bado tunafanya mabadiliko matatu.’

‘Sidhani kama mgomo unaweza kufanyika ama kuna sababu ya kufanya hivyo kwa sababu tunapenda kufurahisha mashabiki wetu. Hata hivyo, mechi za klabu na timu za taifa zimekuwa nyingi sana na likizo kuwa fupi sana. Wachezaji wanahitaji mapumziko ya majuma mawili ama matatu,’ alisema.

Afisa mkuu mtendaji wa Chama cha Wachezaji wa soka ya malipo Uingereza (PFA) Maheta Molango alisisitiza ujumbe wa Guardiola akiongeza kuwa suala hilo halifai kupuuzwa. Aidha, Arsenal itarejea ulingoni hapo kesho ikilenga kuzoa ushindi wake wa nne mfululizo ligini itakapozuru Norwich.

Wanabunduki wa Arsenal walikung’uta Southampton, West Ham na Leeds katika mechi tatu zilizopita. Kocha Mikel Arteta atakuwa na hamu kubwa kuwapa mashabiki wa Arsenal zawadi nzuri ya Krismasi mnamo Desemba 26 ugani Carrow Road.

Hata hivyo, anatarajiwa kukosa huduma za Takehiro Tomiyasu (tatizo la misuli), Calum Chambers, Pablo Mari na Sambi Lokonga (corona), Sead Kolasinac (jeraha la kifundo) naye Pierre-Emerick Aubameyang amekuwa nje kwa sababu za kinidhamu.

You can share this post!

Maelfu wafurika Pwani usalama ukiimarishwa

Wazazi washauriwa kulinda watoto dhidi ya baridi

T L