• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:46 PM
Mkenya Akida ashinda Ligi Kuu ya akina dada Ugiriki

Mkenya Akida ashinda Ligi Kuu ya akina dada Ugiriki

Na GEOFFREY ANENE

MCHEZAJI wa kimataifa wa Kenya, Esse Akida amenyakua taji lake la kwanza kubwa nchini Ugiriki baada kuchangia pakubwa katika kampeni ya AC PAOK kutawala Ligi Kuu ya kinadada ya msimu 2021-2022 ambayo ilikamilika Jumamosi.

Miamba hao kutoka mjini Thessaloniki walipepeta Ergotelis 2-0 katika mchuano wa kufunga msimu kupitia mabao ya Maria Mitkou.

Mitkou alisukuma kombora kali kutoka mbali hadi wavuni dakika ya 32 kabla ya kuongeza bao la pili kutokana na penalti dakika ya 90. Akida alikuwa amekaribia kuongeza la pili dakika ya 65 aliposukuma shuti kutoka nje ya kisanduku, lakini likaondokewa.

Mshambulizi huyo amekamilisha msimu akiwa na mabao 18. PAOK ilisaini Akida mnamo Julai 2021 kwa msimu wa 2021-2022 kutoka Thika Queens. Ilivutiwa na kasi yake, bidii yake, utulivu wake akiwa na mpira na ukatili mbele ya lango.

Akida aliwahi kusajiliwa na Besiktas mnamo Februari 2020, lakini hakuichezea baada ya mkurupuko wa virusi vya corona kusababisha kusimamishwa kwa mashindano kwa muda mrefu.

Nyota huyo aliyewahi kucheza nchini Israel, alisema alipojiunga na PAOK kuwa ndoto yake ni kushiriki Klabu Bingwa Ulaya. Atapata fursa hiyo iwapo PAOK itaongeza kandarasi yake kwa sababu imefuzu kushiriki dimba hilo baada ya kushinda ligi kwa mara ya nane mfululizo na 17 kwa jumla.

  • Tags

You can share this post!

Manifesto: Wanasiasa wahimizwa waweke zingatio kwa sekta ya...

Mchakato wa kuuzwa kwa Chelsea unakamilika rasmi leo Mei...

T L