• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Mkenya Jebet Tirop aweka rekodi mpya ya dunia mbio za kilomita 10 nchini Ujerumani

Mkenya Jebet Tirop aweka rekodi mpya ya dunia mbio za kilomita 10 nchini Ujerumani

Na GEOFFREY ANENE

NYOTA Agnes Jebet Tirop ndiye mshikilizi wa rekodi mpya ya dunia ya mbio za kilomita 10 ya kina dada pekee baada ya kukamilisha umbali huo kwa dakika 30.01 mjini Herzogenaurach nchini Ujerumani.

Katika mashindano hayo yaliyofahamika kama Adizero: Road to Records, Tirop alifuta rekodi ya raia wa Morocco, Asmae Leghzaoui aliyekimbia 30:29 jijini New York nchini Amerika mnamo Juni 8 mwaka 2002.

Mkenya Joyciline Jepkosgei anashikilia rekodi ya dunia ya kilomita 10 ya kinadada ya mbio mseto ya dakika 29:43 kutoka shindano la Birell Prague Grand Prix mwaka 2017.

Hapo Jumapili, vita vya taji la kinadada vilisalia kuwa kati ya Wakenya Sheila Chepkirui na Tirop hatua za mwishomwisho kabla ya Tirop kutawala mzunguko wa mwisho.

Rhonex Kipruto alitwaa taji la wanaume kilomita 10 kwa dakika 26:43. Mkenya huyo anashikilia rekodi ya dakika 26:24 aliyoweka Januari 2020 jijini Valencia, Uhispania.

Wakenya pia walitawala mbio za kilomita 21 kupitia kwa Brenda Jepleting (saa 1:06:52) na Abel Kipchumba (dakika 58:48).

Jacob Krop alibeba taji la kilomita tano kwa dakika 13:06 naye Muethiopia Senbere Teferi akavunja rekodi ya dunia ya wanawake pekee kwa kutimka 14:29 akifuta rekodi ya Mholanzi Sifan Hassan ya 14:44.

Bingwa wa Olimpiki Peres Jepchirchir alikuwa mgeni wa heshima wa mashindano haya yaliyovutia jumla ya wakimbiaji 74 kutoka vitengo vya kilomita tano hadi 21.

You can share this post!

Haaland afunga mabao matatu na kuongoza Dortmund...

Haji arejeshea tena EACC faili za sakata ya Kemsa