• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Mpango wa Crystal Palace kuajiri kocha Lucien Favre wagonga ukuta

Mpango wa Crystal Palace kuajiri kocha Lucien Favre wagonga ukuta

Na MASHIRIKA

KOCHA wa zamani wa Borussia Dortmund, Lucien Favre, amewaeleza Crystal Palace kwamba anatamani kusalia nje ya ulingo wa soka kwa muda mrefu zaidi.

Hii ni baada ya Palace kuanza kuwania maarifa ya mkufunzi huyo kwa nia ya kumfanya mrithi wa Roy Hodgson aliyejieungua uwanjani Selhurst Park mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Mazungumzo kati ya Palace na Favre, 63, yalikuwa yamefikia hatua muhimu na yalikuwa matarajio ya kikosi hicho kumpa Favre mkataba wa miaka mitatu kufikia Juni 27, 2021.

Favre alipigwa kalamu na Dortmund mnamo Disemba 2020, miezi mitano kabla ya Hodgson kuagana na Palace.

Favre anahisi kwamba anahitaji kupumzika zaidi na kujiondoa kwenye ulingo wa soka kwa muda kabla ya kupata nguvu ya kuhamia nchi tofauti, kwa ajili ya ligi mpya na kujifunza lugha nyingine.

Kocha mpya wa Palace atakuwa na kibarua kigumu cha kushawishi wanasoka kadhaa wa haiba kubwa, akiwemo Wilfried Zaha, kusalia uwanjani Selhurst Park kwa muda mrefu zaidi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Madaktari na maafisa bandia wa mifugo Kiambu kuadhibiwa...

Manchester City kumsajili Griezmann iwapo mpango wao wa...