• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Murang’a Seal juu ya jedwali huku Gor ikifinya Ulinzi

Murang’a Seal juu ya jedwali huku Gor ikifinya Ulinzi

NA CECIL ODONGO

MABINGWA watetezi Gor Mahia walidhihirisha ubabe wao baada ya kuliza Ulinzi Stars 1-0 kwenye mechi kali ya Ligi Kuu (KPL) iliyochezewa uga wa Ulinzi Complex Lang’ata Barracks, Nairobi, jana.

Tusker nao jana walitoka nyuma kuagana sare ya 1-1 na Kariobangi Sharks uwanjani Ruaraka, Nairobi.Wageni Murang’a Seal FC walipata ushindi wa pili mfululizo nyumbani baada ya kuilemea Kakamega Homeboyz 1-0 katika uwanja wa St Sebastian Park, Kaunti ya Murang’a.

Gor ambao walitoka 1-1 dhidi ya Sofapaka walionyesha mchezo uliokwenda shule huku wakiwala chenga na kuwazungusha wapinzani wao kama gunia la viazi.

Kiungo Rodgers Mugisha alikuwa kivutio kwa mashabiki kutokana na mchezo mzuri aliouonyesha kwenye mtanange wake wa kwanza.

Gor ilifunga bao hilo la ushindi dakika ya 40 baada ya mabeki wa Ulinzi Stars kukosa kuondoa hatari iliyotokana na kona ya Patrick Sibomana, raia wa Rwanda.

Sajili mpya Kevin Juma aliwahi mpira na kuujaza kimiani huku mashabiki wa Gor akiwemo Waziri wa Mawasiliano Eliud Owalo wakishangilia.

Katika kipindi cha pili, Gor iliendelea kutawala na ilikosa nafasi kadhaa za kutinga mabao ambayo yangewapa ushindi mkubwa.

Katika mechi ya Tusker vijana wa kocha Robert Matano walikimbizwa sana na chipukizi wa Kariobangi Sharks kabla ya Keith Imbali kuwapa Sharks uongozi dakika ya 57.

Tusker walibahatika na kusawazisha pale Sharks walijifunga kutokana na krosi ya beki Levin Odhiambo.

Murang’a Seal nayo jana ilidumisha rekodi ya asilimia 100 ya kushinda mechi zake baada ya kuichapa Kakamega Homeboyz katika uga wa Sebastian Park mjini Murang’a.

Seal ilichapa vijana hao kutoka Kakamega wiki moja tu baada ya kumiminiwa magoli manne na Al- Hilal Benghazi kwenye kipute cha Kombe la Mashirikisho Afrika (CAF).

Mshambuliaji Titus Kapchanga alifunga bao hilo muhimu dakika ya 89 na kuizamisha kabisa chombo cha Homeboyz.

Wachezaji wa Murang’a Seal walisherehekea sana ushindi huo ambao unaonyesha wao ni wakomavu na wanatosha na vijana ambao wamekomaa ligini.

Hii leo, kutakuwa na mechi moja ambapo Nairobi City Stars itapambana na Bidco United katika uwanja wa MISC Kasarani Annex.

 

  • Tags

You can share this post!

Karen Nyamu: Samidoh alinichagua kwa sababu huvalia...

Kongamano: Serikali yaimarisha usalama

T L