• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Muruli aahidi uwazi baada ya kuchaguliwa kuongoza tawi la Kawangware la Ingwe

Muruli aahidi uwazi baada ya kuchaguliwa kuongoza tawi la Kawangware la Ingwe

NA JOHN ASHIHUNDU

JOSEPHAT Muruli Manyonyi ameahidi kuwa na uwazi katika mipango yake ya kuongoza tawi la Kawangware la klabu ya AFC Leopards.

Manyonyi ambaye aliwahi kutekeleza uadhifa huo kati ya 2011 na 2014 alitoa mwito kwa walioshindwa kwenye uchaguzi huo wakubali kusaidiana naye kutimiza malengo yake kulingana na manifesto yake.

“Hata kama haukunipigia kura, ningependa mniunge ili nitimize niliyowaahidi wanachama wakati wa kampeni,” aliongeza.

“Zote tujivunie ushindi huukupitia kwa mwito wangu wa: “Tuanze Fresh- Kazi Bora na Sio Bora Kazi.”

Manyonyi alisema hayo jana baada ya mwishoni mwa wiki kuchaguliwa mwenyekiti mpya wa tawi hilo maarufu.

Uchaguzi huo wa Amani ulifanyika Inxpice Lounge wakati wa Mkutano wa Mwaka (AGM), ambako wanachama walitumia fursa hiyo kuchaguwa maafisa wengine wa kusaidia Manyonyi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Manyonyi amechukuwa usukani kutoka kwa Boniface Anyula ambaye amekuwa akiongoza kwa muda, kufuatia kifo cha Evans Savai aliyeaga mwezi Mei.

Kwenye uchaguzi huo, Manyonyi alishinda kwa kura 47 na kumbwaga, Michael Buleti Imbwaka, aliyepata kura nne pekee. Naibu wake ni Wycliffe Mwanzi aliyechaguliwa bila kupingwa.

Mwenyekiti wa kamati iliyosimamia shughuli hiyo, Julius Shitsama Lukunga alitaganza rasmi Rose Migare Obenda kama mweka hazina baada ya kuhifadhi kiti hicho bila kupingwa.

Kiti cha ukatibu hakikuwaniwa, lakini afisi mpya imepewa idhini ya kuteua mtu wa kujaza nafasi hiyo, baada ya Arnold Andole kukataa kukitetea.

Benard Amboko alichaguliwa bila kupingwa kama Katibu Mtendaji, wakati Judith Anifa Mugaisi akihudumu kama naibu wake baada ya kupata kura 34 na kuwashinda Paul Omukatu na Wycliffe Milembe waliopata kura 15 na nne mtawaliwa. Sophie Abwao na Boniface Shititi walichaguliwa bila kupingwa kama wanakamati.

Maafisa wapya wa tawi la Kawangware ni: Mwenyekiti (Josephat Manyonyi), Naibu-Mwenyekiti (Wycliffe Mwanzi), Mwenyekiti (Rose Migare Obenda), Katibu-Mtendaji (Benard Amboko), Naibu Katibu Mtendaji (Judith Hanifa Mugaisi), Katibu-Mkuu (kuteuliwa na afisi mpya), Wanakamati (Sophie Abwao na Bonfice Shititi)

  • Tags

You can share this post!

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Laikipia

Serikali yaibuka na mikakati ya kushusha gharama ya chakula...

T L