• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 7:55 AM
Mwanatenisi Seline Ahoya atinga nusu-fainali ya Afrika U14 nchini Madagascar

Mwanatenisi Seline Ahoya atinga nusu-fainali ya Afrika U14 nchini Madagascar

NA GEOFFREY ANENE

SELINE Ahoya alimlemea Miranda Ranaivosoa kwa seti mbili kavu katika robo-fainali ya mashindano ya Afrika ya tenisi ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 14 mjini Antananarivo, Madagascar, Ijumaa.

Ahoya, ambaye alimnyamazisha Soa Andriamaniraka kutoka Madagascar katika raundi ya 16-bora 6-1, 6-0 mnamo Septemba 15, alibwaga raia huyo mwingine wa Madagascar kwa alama 6-1, 7-6(2).

Bingwa wa Afrika Mashariki (Zoni ya Nne) wa umri wa wachezaji wasiozidi umri wa miaka 12 na pia 14 Ahoya atakabiliana na Habiba Essam Habib kutoka Misri katika nusu-fainali Septemba 17. Nusu-fainali hiyo inatarajiwa kuwa ngumu, hasa ikilinganishwa kuwa Ahoya na Habiba wanakamata nafasi ya 20 na 24 mtawalia kwenye viwango vya ubora vya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 14 vya Shirikisho la Tenisi barani Afrika (CAT).

Wamisri Dareen Hosam (nambari saba Afrika) na Jina Elmashad (27) watakutana katika nusu-fainali nyingine.

Mashindano hayo yamevutia wachezaji kutoka mataifa ya Kenya, Zimbabwe, Misri, Madagascar na Msumbiji. Ahoya ndiye Mkenya pekee anashiriki. Akishiriakana na Elmashad, wamepepeta Siena Esteves De Sou Figueiredo/Maya Iseline Munguam Awabada 6-0, 6-1 katika nusu-fainali Ijumaa.

  • Tags

You can share this post!

MAPISHI KIKWETU: Donati za chokoleti

TAHARIRI: Serikali irejeshe ruzuku ya mafuta na unga kabla...

T L