• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:55 AM
Mwendeshaji baiskeli Kariuki atawala Migration Gravel Race Maasai Mara

Mwendeshaji baiskeli Kariuki atawala Migration Gravel Race Maasai Mara

Na GEOFFREY ANENE

MKENYA John Kariuki aliibuka mfalme mpya wa mbio za kimataifa za baiskeli za Migration Gravel Race zilizofanyika katika mbuga ya wanyamapori ya Maasai Mara kaunti ya Narok mnamo Juni 18-21.

Taji la akina dada lilinyakuliwa na na Mwitaliano Maria Vittoria Sperotto.

Kariuki alimaliza mikondo yote minne (Mara Training Centre-Majimoto Camp, Majimoto Camp-Marijo, Marijo-Aitong na Aitong-Mara Training Centre) ya jumla ya kilomita 650 kwa saa 20, dakika 24 na sekunde 29. Alishinda mkondo wa kwanza wa kilomita 128 kwa saa 4:13:33 na kukamata nafasi ya tatu katika mkondo wa pili (7:11:00), tatu (3:51:02) na wa nne (5:08:55).

Mkenya Suleman Kangangi, ambaye alikamilisha makala ya kwanza mwaka jana katika nafasi ya pili, alitetemesha katika mkondo wa pili Juni 19 nao Lachlan Morton (Australia) na Jordan Schleck (Uganda) wakatawala mikondo miwili ya mwisho mtawalia.

Katika jedwali la mwisho, Kariuki alifuatwa kwa karibu na Mwitaliano Mattia de Marchi (20:26:46) na Ssekanwagi (21:17:29).Maria alimaliza mashindano kwa saa 24:58:40 akifuatiwa na Mwamerika Lael Wilcox (26:14:33), Berber Kramer (Afrika Kusini) 26:58:15 na Viollette Neza (Rwanda) 28:14:33 katika usanjari huo.

Bingwa wa 2021 kitengo cha kinadada Nancy Akinyi kutoka Kenya aliaga mashindano katika siku ya tatu baada ya kuumia Juni 19.

  • Tags

You can share this post!

KINYANG’ANYIRO 2022: Kaunti ya Kajiado

Biashara sasa zabuni mbinu kuepuka hasara

T L