• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:55 AM
Naibei, Jepchirchir watawala Iten Marathon, watia mfukoni Sh1 milioni

Naibei, Jepchirchir watawala Iten Marathon, watia mfukoni Sh1 milioni

Na FRED KIBOR

SAMUEL Naibei na Caroline Jepchirchir wameibuka washindi wa makala ya kwanza ya mbio za Iten Marathon zilizofanyika kwenye barabara ya Nyaru-Iten, Jumapili.

Naibei alistahimili upepo mkali na baridi katika mbio hizo za kilomita 42 akitwaa taji kwa saa 2:08:43 na kujishindia tuzo ya Sh1 milioni.

Mpinzani wake mkuu Joshua Kogo alikamata nafasi ya pili kwa 2:10:35 naye Albert Kangogo akafunga mduara wa tatu-bora (2:11:46).

Naibei anayetoka Mlima Elgon na kufanyia mazoezi Iten, alifichua kuwa alitumia Iten Marathon kujiandaa kwa Lisbon Half Marathon nchini Ureno mnamo Aprili 2023.

Samuel Naibei akamilisha mbio za kilomita 42 mjini Iten, Jumapili, Desemba 18, 2022. PICHA | FRED KIBOR

“Ushindi umenipatia motisha,” aliongeza mtimkaji huyo mwenye umri wa miaka 29 aliyeshiriki Nakuru City Marathon kitengo cha kilomita 21 majuzi.

Jepchirchir aliwatoka wapinzani wake katika kilomita ya 30 akikata utepe kwa 2:28:33. Alifuatwa kwa karibu na Suzy Chemaimak (2:33:49) na Mary Kipkemoi (2:35:09).

Mshikilizi wa rekodi ya dunia ya 42km ya wanaume Eliud Kipchoge, ambaye alihudhuria mashindano hayo, alipongeza waandalizi akisema yatainua riadha katika eneo la Iten.

“Iten inafahamika kuchangia pakubwa katika ukuaji wa riadha. Hadhi itaongezeka kwa sababu pia kuna marathon. Itakuwa rahisi kuvutia zaidi ya wakimbiaji 1,000 wa kigeni,” alisema Kipchoge aliyeomba wadhamini wajitokeze katika makala yajayo ili kufanikisha mashindano hayo.

Hata hivyo, Kipchoge alieleza kusikitishwa na ongzeko la visa vya matumizi ya dawa za kusisimua misuli nchini na kuonya athari zake ni mbaya.

“Wanariadha wote washinde mbio kwa njia halali na kuna umuhimu mkubwa wa kambi zote za wanariadha na makocha kusajiliwa kuhakikisha mchezo huu unalainishwa na pia kuondoa watu wanaochafua sifa,” alisema.

Gavana wa Elgeyo Marakwet Wisley Rotich alisema kuwa mbio hizo ni mojawapo ya ajenda za serikali yake kusaidia vijana.

Matokeo (10-bora):

Wanaume

Samuel Naibei saa 2:08:43

Joshua Kogo 2:10:35

Albert kangogo 2:11:46

Kennedy Kemboi 2:12:21

William Cheboi 2:13:20

Benson Tunyo 2:14:02

Collins Kipkorir 2:14:46

Stephen Kipkosgei 2:14:56

Isaac Lagat 2:15:10

Silas Too- 2:15:11

Wanawake

Caroline Jepchirchir saa 2:28:33

Suzy Chemaimak 2:33:49

Mercy Kipkemoi 2:35:09

Martha Akeno 2:35:30

Joan Kipyatich 2:36:26

Hilda Cheboi 2:36:46

Janet Kiptoo 2:37:43

Rael Kimaiyo 2:38:28

Hellen Jepkurgat 2:38:29

Faith Jepkoech 2:38:40

TAFSIRI: GEOFFREY ANENE

  • Tags

You can share this post!

Wandayi awataka wakosoaji wa Raila ngomeni Luo Nyanza...

KOMBE LA DUNIA FIFA 2022: Nahodha Luka Modric kuendelea...

T L