• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Namwamba apongeza majagina kwa kujitolea kuimarisha vipaji mashinani

Namwamba apongeza majagina kwa kujitolea kuimarisha vipaji mashinani

NA JOHN ASHIHUNDU

WAZIRI wa Michezo, Ababu Namwamba amewapongeza wanasoka wa zamani waliojitokeza kuimarisha vipaji vya vijana wanaonuia kutimiza ndoto zao mashinani.

Namwamba amesema hayo baada ya kushuhudia mashindano mbali mbali katika sehemu nyingi, hasa katika maeneo ya Magharibi na Nyanza.

Akizungmza kuhusu uaandalizi uliofana wa michauno ya Elijah Lidonde Talent Search katika Kaunti ya Kakamega mwishoni mwa wikendi iliyopita, Namwamba alisema kuna vijana wengi walio na hamu ya kusakata soka, lakini ndoto zao zinazimwa na mipango duni kutoka kwa watu wanaojitakia makuu.

“Serikali itaunga mkono waandalizi wa mashindano ya mashinani ili vijana wengi waimarike na kutimiza ndoto zao. Tutahakikisha viwanja vipi katika hali nzuri, kwa sababu hatuwezi kufaulu kwa sababu hatuna viwanja vya kutosha. Sharti viwanja vyota vya umma vifanyiwe ukarabati,” aliongeza Namwamba ambaye zamani alikuwa afisa wa klabu ya AFC Leopards miaka ya 90s.

Namwamba ambaye aliandamana na maafisa kadhaa kutoka serikali, pamoja na wanasiasa wa tabaka mbali mbali aliwapongeza wanasoka wa zamani wakiongozwa na Washington Muhanji ambao walihusika katika maandalizi ya mashindano ya Elijah Lidonde Talent Search.

Waziri wa Michezo Ababu Namwamva akikabidhi washindi Lurambi FC Kombe la U-17 baada ya kupiga EL Select 3-1. PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Wakati wa mashindano hayo, Lurambi waliibuka mabingwa wa kombe la wasiozidi umri wa miaka 17 baada ya kuwabwaga EL Select 3-1 kwenye fainali iliyofanyika Bukhungu Stadium. Shinyalu walitwaa ubingwa wa kombe hilo kwa upande wa wasichana baada ya kuichapa Lurambi 2-1.

Gavana wa Kakamega Fernandes Barasa akabidhi Shinyalu FC kombe la U-17 walioshinda warembo wa Lurambi 2-1. PICHA | JOHN ASHIHUNDU

Lurambi chini ya kocha Ben Bela Oyalo ilishinda kombe la wasiozidi umri wa miaka 15 baada ya kuizaba EL Select kwa 4-1.

Washindi waliondoka vikombe na vocha za kununua bidhaa madukani, wakati huu wanajiandaa kurejea shuleni Jumatatu baada ya likizo kumalizika wikendi hii.

Chini ya udhamini wa Alex Muteshi ambaye pia ndiye mlezi wa klabu ya AFC Leopards wanasoka wastaafu wameungana kuendeleza Wakfu wa Elijah Lidonde Foundation ambao pia waliandaa mashindano ya watu wazima mwaka uliopita.

Kadhalika, Waziri Namwamba alihudhuria mashindano mbali mbali yakiwa pamoja na Nyadhi Cup katika Kaunti ya Siaya.

Marehemu Lidonde alikuwa nahodha wa timu ya Abaluhya FC sasa AFC Leopards na timu ya taifa ya Kenya miaka ya 50s na 60s kabla ya kustaafu na kuanza kazi ya ukufunzi. Gwigi huyo aliyeaga dunia mnamo aliichezea Kenya mara 26 na kufunga mabao 34.

Wanachama wa Wakfu ya Elijah Lidonde ni Muhanji, Alfred Imonje, Nick Yakhama, Ngaira Esese, Winna Shilavula, Agrrey Litali, Steve Okumu, Tony Lidonde na Fred Serenge.

Dominic Asutsi (mwenye jezi nyeupe) wa Lurambi FC akabwa na mchezaji wa EL Select kwenye fainali ya Elijah Lidonde Talent Search ugani Bukhungu, Kakamega.

  • Tags

You can share this post!

Kerich akamata nafasi ya pili Doha Marathon, Kipchirchir na...

Tenri Joyous Park ilivyo kivutio kwa wanaopenda kutazama...

T L