• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 7:50 PM
Okere ataja 31 kuanza matayarisho ya Harambee Starlets ya Kombe la Afrika dhidi ya Sudan Kusini

Okere ataja 31 kuanza matayarisho ya Harambee Starlets ya Kombe la Afrika dhidi ya Sudan Kusini

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA wa Harambee Starlets, Charles Okere ameamua kuwapa nafasi wazoefu kama Teresa Engesha na Enez Mango katika kikosi chake cha watu 31 kwa mechi dhidi ya Sudan Kusini.

Kikosi hicho kitaingia kambini Oktoba 9 katika hoteli ya Lamada kwa mechi za raundi ya kwanza za kufuzu kushiriki Kombe la Afrika (AWCON) zitakazosakatwa Oktoba 20 na Oktoba 24 jijini Nairobi.

Okere atakuwa na kibarua kigumu kutaja kikosi cha mwisho, hasa katika idara ya ushambuliaji iliyo na wakali Engesha, Jentrix Shikangwa, Lucy Mukhwana, Mwanahalima Adam, Rachael Muema na Violet Wanyonyi.

Mshindi kati ya Kenya na Sudan Kusini atakabiliana na mshindi kati ya Uganda na Ethiopia katika raundi ya pili. Atakayeshinda raundi ya pili atajikatia tiketi ya kushiriki AWCON 2022 nchini Morocco.

Kenya imeshiriki AWCON mara moja pekee, mwaka 2016. Kipa Lilian Awuor, beki Dorcas Shikobe, viungo Corazone Aquino, Lydia Akoth na Janet Bundi ni baadhi ya wachezaji walio kikosini ambao pia walikuwa AWCON 2016 nchini Cameroon.

Kikosi cha Harambee Starlets

Makipa – Annete Kundu (hana klabu), Pauline Katharu (Kibera Girls Soccer), Lilian Awuor (Vihiga Queens), Maureen Shimuli (Ulinzi Starlets);

Mabeki – Vivian Nasaka (Vihiga Queens), Juliet Adipo (Kayole Starlet), Dorcas Shikobe (Lakatamia FC), Lucy Akoth (Mathare United Women FC), Dorcas Neema (Nakuru Queens), Phoebe Awiti

(Vihiga Queens), Enez Mango (Vihiga Queens), Nelly Sawe (Thika Queens), Ruth Ingotsi (hana klabu);

Viungo – Sheril Angachi (Gaspo Women), Corazone Aquino (Gaspo Women), Mercy Oginga (Vihiga Queens), Lydia Akoth (Thika Queens), Lilian Mmboga (Kibera Girls Soccer), Lorna Nyarinda (Kibera Girls Soccer), Martha Amunyolet (Trans Nzoia Queens), Maureen Ater (Vihiga Queens), Merceline Wayodi (Kisumu All Starlets);

Washambuliaji – Teresa Engesha (Vihiga Queens), Rachael Muema (Thika Queens), Janet Bundi (Vihiga Queens), Jentrix Shikangwa (Vihiga Queens), Lucy Mukhwana (Ulinzi Starlets), Neddy Akoth (Ulinzi Starlets), Mwanahalima Adam (Thika Queens), Violet Wanyonyi (Vihiga Queens), Elizabeth Wambui (Gaspo Women FC).

You can share this post!

Gideon Moi awakosha roho mabwanyenye wa Mlima Kenya huku...

MKF yasema haijaamua ni nani itaunga mkono