• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 4:32 PM
Olunga, Al Duhail waandaliwa chakula cha mchana na kiongozi wa Qatar katika kasri lake

Olunga, Al Duhail waandaliwa chakula cha mchana na kiongozi wa Qatar katika kasri lake

Na GEOFFREY ANENE

NAHODHA wa Harambee Stars Michael Olunga ameshukuru Kiongozi wa Qatar, Tamim bin Hamad Al Thani kwa kuandalia klabu ya Al Duhail dhifa ya mchana mnamo Machi 20.

Al Duhail ilimtembelea kiongozi huyo katika kasri lake baada ya kutwaa ubingwa wa Amir Cup katika maadhimisho ya miaka 50 tangu kombe hilo lianzishwe.

Ilipepeta Al Gharafa 5-1 Machi 18 kupitia mabao ya Edmilson Junior, Olunga, Almoez Ali, Ferjani Sassi na Abdeirahman Moustafa uwanjani Khalifa ambao ni moja ya viwanja vitakavyotumiwa kwa Kombe la Dunia baadaye 2022.

“Chakula cha mchana katika kasri la Kiongozi wa Qatar baada ya kuibuka washindi wa Amir Cup 2022. Ni heshima kubwa,” alisema mshambulizi Olunga kupitia mitandao yake ya kijamii.

Al Duhail iliongeza, “Ni heshima kubwa kutembelea kiongozi wetu baada ya kushinda Kombe la Amir na pia kumaliza Ligi Kuu katika nafasi ya pili. Heshima hii ni motisha kwetu sote kuwa wabunifu na kutafuta mafanikio michezoni.”

Olunga aliibuka mfungaji bora ligini baada ya kutetemesha nyavu za wapinzani mara 24.

You can share this post!

Serikali yahimiza maombi kwa ajili ya amani nchini

Siasa zazima uwezo wa serikali kuweka sheria

T L