• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Orao: Tuna uwezo kujiondoa mduara hatari

Orao: Tuna uwezo kujiondoa mduara hatari

Na JOHN KIMWERE

KOCHA wa Kangemi Starlets, Joseph Orao amesema wana uwezo wa kujituma na kujiondoa kutoka mduara wa kushushwa ngazi kwenye kampeni za Ligi Kuu ya Soka la Kenya (KWPL).

Orao amedokeza kuwa timu hiyo ilijumuisha idadi kubwa ya wachezaji wa shule waliowasaidia kufuzu kushiriki ngarambe hiyo. ”Baada ya kupanda ngazi iliibuka kuwa vigumu kutumia huduma za wachezaji hao kutokana na shughuli za masomo,” alisema na kuongeza hali hiyo imechangia kikosi hicho kutofanya vizuri kwenye kampeni za kipute cha muhula huu.

Kampeni za kipute hicho sio mteremko wamepata ushindani mkali dhidi ya wapinzani wao. Anasema kuwa ni aibu kubwa kupanda ngazi na kushushwa ngazi baada ya msimu mmoja. ”Kusema ukweli hauwezi kulinganisha mechi za Ligi ya Taifa Daraja la Kwanza na kampeni za KWPL,” akasema.

Kangemi Starlets imetwaa huduma za wachana nyavu wawili, Esther Atieno na Rebecca Odato wanafunzi wa kidato cha kwanza kwenye Shule ya Dagoretti Mixed. Anadokeza kuwa wanalenga kusajili wachezaji kadhaa kabla ya mechi za mkumbo wa pili kuanza wikendi ijayo.

Baada ya kushiriki mechi kumi, Kangemi imevuna alama tatu kwa kushinda patashika moja na kupoteza mara tisa ambapo inavuta mkia kwenye jedwali. Vihiga Queens inaongoza kwa kuzoa alama 28, saba mbele ya Gaspo Women. Thika Queens inafunga tatu bora kwa kuvuna pointi 20, moja mbele ya Ulinzi Starlets.

You can share this post!

Thika Queens yajinolea CECAFA

Leopards yatandika Dandora Love 6-1 mechi ya kirafiki

T L