• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 5:04 PM
Pelicojam yapania kushiriki kipute cha Afrika mashariki na kati

Pelicojam yapania kushiriki kipute cha Afrika mashariki na kati

Na JOHN KIMWERE

JAMHURI High School FC (PELICOJAM FC) ni kati ya timu ambazo hufanya vizuri kwenye mashindano ya michezo baina ya shule za Upili nchini.

Aidha ni miongoni mwa vikosi vinavyoshiriki mechi za Ligi ya Kaunti kwa Mara ya tano ambazo huandaliwa na Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) Tawi la Nairobi Magharibi. Kwenye shindano la Afrika Mashariki na Kati inajivunia kushiriki mara moja.

Ingawa kikosi cha Dagoretti High School kimekuwa tisho kwenye mashindano hayo katika Kaunti ya Nairobi na kote nchini kwa jumla imepania kupambana kwa udi na uvumba kuhakikisha inatwaa tiketi ya kuwakilisha Kenya kwenye ngarambe ya Afrika Mashariki na Kati baadaye mwaka huu.

”Tunashuruku uongozi wa shule yetu ambapo tumepata sapoti tosha kitengo cha michezo kwa jumla,” msimamizi wa michezo shuleni humo, Justus Akhwesa alisema na kuongeza kuwa mwaka huu wamepania kujituma kiume ili kuhakikisha wamefanya kweli kwenye michezo ya shule na FKF. ”

Tuna wachezaji wazuri wa kidato cha kwanza hadi cha tatu ambapo tuna imani wanatosha mboga kufanya kweli kwenye michezo ya shule kitaifa na kufuzu kushiriki ngarambe ya Afrika Mashariki na Kati kwa mara ya pili,” akasema.

Timu ya Jamhuri High School FC…Picha/JOHN KIMWERE

MWAKA 2010

Jamhuri High School ilishiriki kipute hicho mara moja mwaka 2010 ilipomaliza ya pili baada ya kupigwa na St Mary Kitende. Miaka yote Jamhuri hushindwa kufuzu kushiriki kipute hicho ambapo hubanduliwa katika fainali na Dagoretti High.

Mara mbili kwenye shindano la shule za upili yaliyoandaliwa mwishoni mwa mwaka jana na mapema mwaka huu Jamhuri High ilimaliza ya pili ilipozimwa na Dagoretti High kwa mabao 2-1 na 5-1 mtawalia. Naye kocha mkuu, Fredrick Amolo anasema ”Msimu huu tumepania kujituma mithili ya mchwa kwenye mechi za ligi nia yetu ikiwa kumaliza kati ya nafasi tatu bora na kupandishwa ngazi kushiriki ngarambe ya Regional League muhula ujao.”

Jamhuri High imepangwa Kundi A kwenye ngarambe ya Ligi ya Kaunti linalojumuisha wapinzani wengine kama Kangemi Patriots, Young City, Kipande FC, Re Union na UoN Olympic kati ya zingine. Leo kikosi hicho kimepangwa kucheza dhidi ya Kenya Forest Service (KFS).

Kocha huyo ambaye amefundisha kikosi hicho kwa kipindi cha miaka 12 husaidiana na naibu wake Curtis Juma. Kwenye kampeni za kinyang’anyiro hicho muhula uliyopita Jamhuri High School ilimaliza ya nne katika jedwali na kukosa pembamba kutwaa tiketi ya kupandishwa ngazi msimu huu.

Jamhuri High inajivunai kunoa makucha ya wachezaji wengi ambao wamefanikiwa kuteuliwa na klabu ambazo hushiriki ligi tofauti nchini.

IMEKUZA

Baadhi yao wakiwa: John Oyemba yupo Norway, Nixon Omondi (Sofapaka FC), Robison Kamura (KCB), Antony Odinga (Mathare United), Enock Momanyi (FC Talanta), Eric Mmata (Kariobangi Sharks), Curtis Juma (Zetech Titans), Clinton Oseko (Liberty FC) na Victor Otieno (AFC Leopards). Wengine wakiwa Patrick Mugendi aliyekuwa akichezea Bandari FC na Brian Birigen (Ulinzi Stars).

Jamhuri High inashirikisha: Griffins Ochieng na Jonathan Wise (nahodha na naibu wake), Salim Hassan, Mark Otieno, Derrick Wahome, Simon Ndombi, Stephen Otieno, Hannington Wandabwa, Alex Otieno, Abdiaziz Mohamed.

Jackson Otieno, Brian Mdiku, Weber Hugues, Giggs Kamau, Referendum Muthengi, Fred Tuyishime na Ayub Mwita. Pia wapo Clive Billy Ocean, Trevor Omondi, Edward Odhiambo, Edmond Olak, Emmanuel Otieno, Abdulmajid Jimasho, Gerison Oyoo, Adrian Mwaura, Miradi Tumba, John Shimirimana, Romeo Otieno, Adrian Muuo, Gregory Otieno, Isaiah Bumatet na Isham Gutam.

Timu ya Jamhuri High School FC…Picha/JOHN KIMWERE

You can share this post!

Maeneo yatakayoamua wazito kaunti za Pwani

Unachotakiwa kufanya ili kuondoa mba kichwani

T L