• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 9:01 PM
Peru yakomoa Venezuela na kuingia robo-fainali za Copa America

Peru yakomoa Venezuela na kuingia robo-fainali za Copa America

Na MASHIRIKA

PERU walikamilisha kampeni za Kundi B kwenye Copa America katika nafasi ya pili na kufuzu kwa hatua ya nane-bora baada ya kuwacharaza Venezuela 1-0 mnamo Jumapili usiku nchini Brazil.

Chini ya kocha Ricardo Gareca, Peru waliofungiwa bao na Andre Carrillo dhidi ya Venezuela, walijizolea alama saba kutokana na mechi nne kundini. Ni pengo la pointi tatu pekee ndilo linatamalaki kati yao na Brazil walioshinda mechi tatu na kuambulia sare mara moja.

Zaidi ya Peru na Brazil ambao ni mabingwa watetezi na wenyeji wa Copa America, vikosi vingine ambavyo tayari vimefuzu kwa hatua ya robo-fainali ni Colombia na Ecuador ambavyo vilitia kapuni alama nne na tatu mtawalia.

Venezuela waliaga mapema mashindano ya Copa America mwkaa huu baada ya kujizolea alama mbili pekee kutokana na mechi nne za hatua ya makundi.

Peru walifungua makala ya 47 ya Copa America kwa kupokezwa kichapo kinono cha 4-0 kutoka kwa Brazil mnamo Juni 18. Mabao yao katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Colombia yalipachikwa wavuni kupitia Sergio Pena na beki wa Everton, Yerry Mina aliyejifunga.

Kabla ya kushuka dimbani kuvaana na Venezuela, walikuwa wamewalazimishia Ecuador sare ya 2-2 katika mechi ya tatu ya Kundi B.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Pigo kwa Croatia corona ikimweka nje fowadi tegemeo Ivan...

Serikali kuhakikisha wakazi wa mitaa ya mabanda wanapata...