• Nairobi
  • Last Updated September 28th, 2023 10:25 PM
Phil Foden kukosa mechi tatu za kwanza za Manchester City kwa sababu ya jeraha

Phil Foden kukosa mechi tatu za kwanza za Manchester City kwa sababu ya jeraha

Na MASHIRIKA

KIUNGO Phil Foden atakosa mechi kadhaa za kwanza za Manchester City katika msimu mpya wa 2021-22 kutokana na jeraha la mguu alilopata wakati wa fainali ya Euro 2020 iliyokutanisha Uingereza na Italia mnamo Julai 2021.

Foden, 21, anatarajiwa sasa kukosa michuano mitatu ijayo dhidi ya Tottenham Hotspur, Norwich City na Arsenal.

Kiungo huyo huenda pia akakosa mechi ya kufuzu kwa Kombe la Dunia la 2022 dhidi ya Hungary mnamo Septemba 2021.

“Foden atasalia nje kwa zaidi ya wiki nne. Hivyo, huenda mchuano wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) msimu huu ukawa dhidi ya Leicester City mnamo Septemba 11,” akasema kocha Pep Guardiola wa Man-City.

Guardiola pia amethibitisha kwamba Man-City wataanza kampeni za muhula ujao wa 2021-22 bila kiungo Kevin de Bruyne ambaye alipata jeraha la kifundo cha mguu kwenye robo-fainali ya Euro 2020 dhidi ya Italia.

Mnamo 2021-22, Leicester walishinda taji la EPL na kutinga fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Kocha Marcelo Bielsa arefusha muda wa kuhudumu kwake Leeds...

Machifu kuaga afisi za kikoloni