• Nairobi
  • Last Updated May 13th, 2024 5:30 PM
Pogba asema wezi walitoweka na medali yake ya ushindi wa Kombe la Dunia

Pogba asema wezi walitoweka na medali yake ya ushindi wa Kombe la Dunia

Na MASHIRIKA

KIUNGO Paul Pogba wa Manchester United amesema wezi waliovamia makazi yake walitoweka na medali yake ya ushindi wa Kombe la Dunia mnamo 2018.

Pogba, 29, alizungumzia tukio la kuhofisha ambalo familia yake ilikabiliana nalo wiki iliyopita baada ya majambazi kuvamia makazi yake alipokuwa akichezea Man-United dhidi ya Atletico Madrid katika marudiano ya gozi la Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) ugani Old Trafford.

Wakati wa uvamizi huo, watoto wake wawili wadogo walikuwa na mfanyakazi wao wa nyumbani pekee.

“Muhimu zaidi ni kwamba hawakudhuru watoto wangu. Wote wako salama,” akasema Pogba alipokuwa akihojiwa na wanahabari wa kituo cha Le Figaro nchini Ufaransa.

Ufaransa walishinda Kombe la Dunia mnamo 2018 baada ya kutandika Croatia 4-2 kwenye fainali iliyoandaliwa jijini Moscow, Urusi. Pogba alifungia kikosi chake bao la tatu.

“Vitu vingine vilivyoibwa ni vito vya thamani vya mamangu,” akasema Pogba.

Pogba alirejea Man-United mnamo 2016 baada ya kuagana na Juventus ya Italia kwa ada ya Sh12.4 bilioni iliyomfanya mchezaji ghali zaidi nchini Uingereza.

Nyota huyo kwa sasa yuko Ufaransa anakotarajiwa kuongoza timu yake ya taifa kuvaana na Ivory Coast ba Afrika Kusini kirafiki.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

UJASIRIAMALI: Amefuma vikapu karibu miaka 40 na nguvu bado...

Wanasiasa wanawake kufundishwa kujikinga na dhuluma...

T L