• Nairobi
  • Last Updated May 3rd, 2024 11:33 PM
Rashford kukaa nje kwa miezi miwili akiamua kufanyiwa upasuaji kwenye bega

Rashford kukaa nje kwa miezi miwili akiamua kufanyiwa upasuaji kwenye bega

Na MASHIRIKA

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

MSHAMBULIAJI Marcus Rashford huenda akakosa kuwajibikia waajiri wake Manchester United kwa kipindi cha miezi mitatu ijayo iwapo atafanyiwa upasuaji wa bega.

Kwa mujibu wa kocha Ole Gunnar Solskjaer, sogora huyo raia wa Uingereza bado ‘anawazia’ iwapo atafanyiwa upasuaji huo mwisho wa mwezi huu au la.Japo Rashford amekuwa akitatizwa na jeraha la bega kwa miezi saba iliyopita, fowadi huyo alikuwa sehemu ya kikosi kilichotegemewa na Uingereza kwenye fainali zilizopita za Euro.

Rashford aliwajibishwa na kocha Gareth Southgate katika michuano mitano ya Euro 2020 na alikuwa miongoni mwa chipukizi watatu wakiwemo Jadon Sancho na Bukayo Saka waliokabidhi Italia ubingwa wa taji hilo baada ya kupoteza penalti kwenye fainali.

Solskjaer amekiri kwamba Rashford aliondoka ghafla kambini mwao kabla ya Man-United kushuka dimbani Jumapili kupimana nguvu na Derby County inayonolewa na sogora wao wa zamani, Wayne Rooney.Man-United walisajili ushindi wa 2-1 kwenye mechi hiyo.

Walifunga magoli yao kupitia tineja raia wa Uruguay, Facundo Pellistri, 19, pamoja na Tahith Chong ambaye atatumwa kuchezea Birmingham City kwa mkopo mnamo 2021-22.“Rashford alifanyiwa tathmini na mtaalamu wa afya wiki iliyopita.

Anahisi kwamba njia ya pekee ya kukabiliana na jeraha ambalo limemtatiza kwa miezi saba sasa ni upasuaji,” akatanguliza Solskjaer.“Aliondoka kambini kwenda kuliwazia suala hilo la upasuaji kwa muda zaidi. Italazimu tufanye jambo ambalo litakuwa jema kwake na bora kwa klabu. Tutawahusisha wataalamu zaidi,” akaongeza mkufunzi huyo raia wa Norway.

Solskjaer alikuwa pia mwingi wa sifa kwa wanasoka Tom Heaton na Jesse Lingard aliyerejea ugani Old Trafford mwishoni mwa msimu wa 2020-21 baada ya kipindi chake cha mkopo kambini mwa West Ham United kukamilika.

“Lingard anataka kupigania upya nafasi yake kikosini. Lingard tuliyemuona West Ham msimu jana ndiye Lingard wa kweli. Kwa sasa yuko katika sehemu ya mipango yangu msimu ujao,” akasema Solskjaer.

 

  • Tags

You can share this post!

Rashford kukaa nje kwa miezi miwili akiamua kufanyiwa...

Rangers kukutana na Malmo au HJK Helsinki katika mchujo wa...