• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 1:15 PM
Real, Barcelona na Juventus watetea kuhusika kwao kwenye kipute cha European Super League (ESL)

Real, Barcelona na Juventus watetea kuhusika kwao kwenye kipute cha European Super League (ESL)

Na MASHIRIKA

REAL Madrid, Barcelona na Juventus wametetea mipango yao ya kuingia katika kipute kipya cha European Super League (ESL) huku wakikashifu vinara wa Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa) kwa “vitisho visivyokuwa na mashiko”.

Klabu hizo tatu ndizo za pekee kati ya 12 zilizoingia ESL ambazo bado hazijajiondoa kwenye kivumbi hicho huku wakikabiliwa sasa na adhabu kali kutoka kwa Uefa.

Klabu tisa nyinginezo, zikiwemo sita kuu za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), tayari zimeadhibiwa vikali ambapo watatozwa faini na kunyima mapato yatakayotokana na ushiriki wao wa kipute cha Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo 2023-24.

“Klabu zilizoanzisha kipute cha ESL zimeumia sana kifedha,” wakasema Barcelona, Real na Juventus kwenye taarifa ya pamoja.

“Tumekuwa tukiwa presha kutoka kwa wadau mbalimbali na kupokea vitisho ili kutupilia mbali mpango na pendekezo la kuunda kivumbi cha ESL kwa sababu ya ubinafsi na ukiritimba wa watu wachache wasiopenda maendeleo ya soka barani Ulaya na duniani kwa jumla,” ikaendelea taarifa hiyo.

Mpango wa kuanzishwa kwa soka ya ESL ulitangazwa mnamo Aprili 18 japo ukapokelewa kwa hisia mseto na wadau. Chini ya kipindi cha saa 48 baada ya kutangazwa kwa kipute hicho, vikosi vyote sita vya EPL vilivyohusishwa vilijiondoa huku maandamano ya mashabiki nje ya viwanja vya klabu hizo yakishuhudiwa nchini Uingereza.

Mnamo Jumamosi, vinara wa vikosi tisa vilivyojiondoa kwenye kipute cha ESL – Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Tottenham Hotspur, AC Milan, Inter Milan na Atletico Madrid walisema kwamba watafanya kila liwezekanalo kutamatisha kuhusika kwao kwenye kivumbi cha ESL na kuaminisha mashabiki wao kwamba wamelizika kabisa suala hilo katika kaburi ya sahau.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Barcelona na Atletico Madrid nguvu sawa katika Ligi Kuu ya...

Maandamano yaendelea Chad wiki kadhaa baada ya kifo cha...