• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 10:50 AM
Refa Alex Kenyani anayepania kuwa kama Mike Dean

Refa Alex Kenyani anayepania kuwa kama Mike Dean

Na PATRICK KILAVUKA

Urefa faafu wa Mark Dean ambaye anapuliza kipenga katika michuano ya bara uropa Ligi ya EPL ni kichocheo cha muamuzi wa kati Alex Kenyani.

Mbali na kwamba, mbegu ya urefa wake imenawiri kwenye rutuba mzuri na kupaliliwa kuzaa mazao ya mataji katika vipute mashinani kwa kuwa refa bora. Hata hivyo, umakinifu wake umemwezesha kupanda ngazi hatua kwa hatua na sasa anachezesha Ligi za Daraja na Kwanza na ya Pili ya Shirikisho la Soka Kenya.

“Nimechezesha Ligi ya Daraja ya Pili kwa miaka minne kabla kupandisha ngazi kuchezesha Ligi ya Daraja ya Kwanza mwaka 2020, ” anasema muamuzi huyo wa kati ambaye huchezesha pia michuano ya mashule na vyuo pamoja na vipute. Amewahi kutuzwa kama refa bora katika vipute vya Tim Wanyonyi Super Cup mwaka 2018 na cha 2021 ambacho kilijulikana kama Westlands Youth Soccer Tournment.

Alichezesha mchuano wa fainali dhidi ya Leads United dhidi ya Wazoefu ambapo United ilipiga wapinzani hao matuta 4-2 baada ya sare tasa muda wa kawaida. Isitoshe, alituza muamuzi wa bora katika patashika la Koth Biro, 2019. Kabla kuwa refa, alikuwa mchezaji wa pembeni wa kushoto.

Alizaliwa Mbale, Kaunti ya Vihiga akiwa mwana wa pili miongoni mwa wana watatu wa Bw. Fanuel Aduvaga na Bi. Grace Munagi. Alisomea shukle ya Msingi na Upili ya Mbihi. Alianza kucheza kama difenda akiwa na miaka 14 kabla kuchongwa kipawa chake zaidi katika timu ya mtaani ya Mbihi Rangers ambayo ilicheza Ligi ya wilaya ya Vihiga.

Refa Alex Kenyani almaarufu “mrefu” akimjulisha mfadhili wa kipute cha Westlands Youth Soccer Tournment Mheshimiwa Tim Wanyonyi marefa wenzake kabla kupiga fainali ya kinganganyiro – Leads United dhidhi ya Wazoefu, uwanajani Kihumbuini…Picha/PATRICK KILAVUKA

Alipata fursa ya kutambisha soka alipokuja Nairobi na kujiunga na timu ya Brookside FC na kuichezea kwa mitano kutoka 2000-05. Baada ya kuchezea Brookside, alipata kibarua cha kazi ya Useremala mwaka 2006 kwa Kapila Mugo kabla kufungua kazi yake 2010.

Akiwa akiwa anafanya kazi ya useremala, kiu ya kuwa muamuzi wa kabumbu kilimsakama na alikumbatiwa na refa Aggrey Shavera( aliye mwenyekiti wa marefa wa FKF, Nairobi West). Alimshika mkono hadi akapata kozi ya urefa na sasa ni mmiliki wa chati cha daraja ya tatu cha FKF kwa mustakabali wa Fifa.

Mpuliza kipenga Kenyani “mrefu” anasema kutokana na kuwa makini uwanjani, refa hufanya maamuzi bora hupaswa kuwajibika ipasavyo katika kutekeleza wajibu wake kwani, macho uwanjani humwaangulia na yeye ni kioo cha mashabiki na timu ambazo zinashiriki ngarambe ambapo maamuzi yasiofaa yaweza kuzua sintofahamu ya atiati na kuzusha hali tete.

“Ukichezesha mechi pasi na kuonea, kwa haki na usawa utaepuka lawama! Isitoshe, kuwa makini na kuepukana suala la ufisadi mwisho wa siku kazi yako hujitokeza kuwa shwari na uchezeshaji wako hujiongea thamani,” adokeza refa huyo asiyependa kutiwa doa kwa kutekeleza haki ya machakato kuleta uhondo viwanjani.

Yeye ni shabiki shupavu wa timu ya Arsenal. Changamoto amewahi kukabiliana nayo alipoanza safari ya urefa ni matusi ya mashabiki ambao hawakosi visa vya utovu wa nidhamu wala rabsha. Angependa kuona refa na marefa wasaidizi wakishirikiana sako kwa bako ugani kutekeleza wajibu wao kwa njia mufti ili pande zote ziridhike kwamba, boli ilitamba kwa njia bora.

Wakati wake ambao anafurahia kuchapa kazi ya kufurahishwa sana ni fainali ya mwaka jana (2021) ya Westlands Youth Soccer Tournment (Tim wanayonyi Super Cup) ambapo alitawazwa mpuliza firimbi bora kwenye ngarambe ambayo ilisisimua sana.

Refa Alex Kenyani almaarufu “mrefu” akipokea tuzo lake baada ya kutawazwa muamuzi bora wa kipute cha Westlands Youth Soccer Tournment, 2021 amabcho kilifadhili na Mheshimiwa Tim Wanyonyi uwanajani Kihumbuini…Picha/PATRICK KILAVUKA

You can share this post!

PENZI LA KIJANJA: Sigeuze bedirumu afisi yako!

Equatorial Guinea yaning’iniza Algeria pembamba...

T L