• Nairobi
  • Last Updated May 22nd, 2024 4:47 PM
Ryan Bertrand sasa ni mali rasmi ya Leicester City baada ya kuondoka Southampton

Ryan Bertrand sasa ni mali rasmi ya Leicester City baada ya kuondoka Southampton

Na MASHIRIKA

RYAN Bertrand, 31, amejiunga na Leicester City kwa mkataba wa miaka miwili huku akiwa huru kurefusha kandarasi hiyo kwa miezi 12 mingine uwanjani King Power.

Nyota huyo ambaye amechezea timu ya taifa ya Uingereza mara 19 hakuwa na klabu baada ya kuachiliwa na Southampton mnamo Juni 30, 2021. Hadi mkataba wake ulpokatika uwanjani St Mary’s, Bertrand alikuwa amechezea kikosi hicho mara 240 katika kipindi cha miaka saba.

Hadi alipoamua kutua Leicester ya kocha Brendan Rodgers, Bertrand alikuwa pia akihemewa na Arsenal ambao kwa sasa wanamvizia beki matata wa Benfica, Nuno Tavares.

Kusajiliwa kwa Bertrand kunachochewa na ulazima wa Leicester kujaza pengo lililoachwa na veteran Christian Fuchs aliyeondoka uwanjani King Power mwishoni mwa msimu huu wa 2020-21.

Luke Thomas, 20, ambaye ni chipukizi wa zamani wa Leicester, anatarajiwa sasa kushirikiana na Bertrand pamoja na Timothy Castagne ambaye amekuwa akiwajibishwa pakubwa katika nafasi iliyoachwa wazi na Ben Chilwell aliyesajiliwa na Chelsea mnamo 2020-21.

Bertrand alianza kusakata soka kitaaluma akivalia jezi za Chelsea baada ya kuagana na Gillingham mnamo 2005.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Itakuwa moto Italia, Ubelgiji zikikwaruzana robo ya Euro...

Viongozi wa Kiislamu washutumu TSC kutoajiri walimu wengi...