• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 6:40 PM
Salah na Kerr waibuka wachezaji bora wa tuzo za Shirika la Waandishi wa Soka (FWA)

Salah na Kerr waibuka wachezaji bora wa tuzo za Shirika la Waandishi wa Soka (FWA)

Na MASHIRIKA

FOWADI Mohamed Salah wa Liverpool mwanasoka bora wa kiume wa tuzo ya Shirika la Waandishi wa Soka (FWA) huku Sam Kerr wa Chelsea akitwaa tuzo hiyo kwa upande wa wanawake.

Salah ambaye ni raia wa Misri, amefungia Liverpool mabao 30 kufikia sasa msimu huu, yakiwemo 22 katika Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). Ufanisi huo unaweka hai matumaini ya waajiri wake kukamilisha kampeni za muhula huu wakijivunia jumla ya mataji manne kabatini mwao – Carabao Cup, EPL, Kombe la FA na Klabu Bingwa Ulaya (UEFA).

Kerr ambaye ni raia wa Australia, amefungia Chelsea mabao 18 katika Ligi Kuu ya Soka ya Wanawake nchini Uingereza (WSL) na kuweka hai matumaini ya kikosi hicho kutawazwa mabingwa wa kipute hicho msimu huu.

Salah, 29, alitawazwa mshindi wa tuzo ya FWA mnamo 2018 na alikuwa sehemu ya kikosi kilichotandika Chelsea kwa penalti 11-10 mwishoni mwa Februari 2022 na kunyanyua taji la Carabao Cup ugani Wembley.

Kwa upande wake, Kerr, 28, kwa sasa ndiye anaongoza orodha ya wafungaji bora wa WSL msimu huu na amesaidia Chelsea kufuzu kwa fainali ya Kombe la FA itakayowakutanisha na Manchester City mnamo Mei 2022.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Ashtakiwa kwa kumtwanga aliyekuwa mke wake siku za nyuma

Wakala wa soka, Mino Raiola, aaga dunia akiwa na umri wa...

T L