• Nairobi
  • Last Updated May 10th, 2024 6:24 PM
Wakala wa soka, Mino Raiola, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 54

Wakala wa soka, Mino Raiola, aaga dunia akiwa na umri wa miaka 54

Na MASHIRIKA

MINO Raiola, ajenti aliyewakalisha baadhi ya wanasoka wa haiba kubwa zaidi duniani, amefariki akiwa na umri wa miaka 54.

Baadhi ya wanasoka waliokuwa wateja wa Raiola aliyekuwa raia wa Uholanzi na Italia ni Erling Haaland wa Borussia Dortmund, Paul Pogba wa Manchester United na Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan.

Hadi kifo chake, Raiola alikuwa pia rais wa Football Forum, shirika lililojumuisha baadhi ya mawakala maarufu wa soka na wachezaji wao.

“Tutakosa uwepo wake daima. Ameacha pengo kubwa,” ikasema sehemu ya taarifa ya familia ya Raiola.

“Tumesikitishwa pakubwa na kuaga kwake. Alikuwa ajenti wa soka aliyejali familia na kupenda mchezo,” ikaendelea taarifa hiyo.

“Raiola alipigana hadi kifo chake kwa nguvu sawa na ile aliyozoea kuelekeza kwenye meza ya kupigania maslahi ya wanasoka wetu duniani,” ikaongeza taarifa.

Raiola aliwahi pia kuwa wakala wa fowadi Mario Balotelli wa Italia na beki matata raia wa Uholanzi, Matthijs de Ligt. Kutokana na kazi yake, aliwahi kutofautiana pakubwa na baadhi ya wakufunzi akiwemo Alex Ferguson (Manchester United), Pep Guardiola (Manchester City) na  Jurgen Klopp (Liverpool).

Mnamo 2021, alikiri kwamba alikuwa amejifunza mengi kutokana na matukio yaliyomfanya kutofautiana na makocha kadhaa katika ulingo wa soka.

Iliwahi kudaiwa kwamba Raiola alitia mfukoni kima cha Sh6.3 bilioni baada ya kufanikisha uhamisho wa Pogba kutoka Juventus hadi Man-United kwa Sh12.4 bilioni mnamo 2016.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Salah na Kerr waibuka wachezaji bora wa tuzo za Shirika la...

Liverpool wakomoa Newcastle na kuweka hai matumaini ya...

T L