• Nairobi
  • Last Updated May 20th, 2024 9:16 PM
Shaqiri atia saini mkataba wa miaka mitatu kambini mwa Lyon

Shaqiri atia saini mkataba wa miaka mitatu kambini mwa Lyon

Na MASHIRIKA

KIUNGO matata raia wa Uswisi, Xherdan Shaqiri sasa ni mali rasmi ya Olympique Lyon baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Liverpool kwa Sh1.5 bilioni.

Shaqiri, 29, ametia saini mkataba wa miaka mitatu na Lyon ambayo inashiriki Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1).

Aliingia kambini mwa Liverpool mnamo 2018 baada ya kuagana na Stoke City kwa Sh2 bilioni. Hata hivyo, aliwajibishwa na kocha Jurgen Klopp mara tano pekee katika michuano ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) mnamo 2020-21.

Nyota huyo wa zamani wa Bayern Munich na Inter Milan alisaidia Liverpool kunyanyua taji la EPL na Klabu Bingwa Ulaya katika kipindi cha kuhudumu kwake ugani Anfield.

Anakuwa mchezaji wa pili wa Liverpool kujiunga na kikosi cha Ligue 1 muhula huu baada ya kiungo matata raia wa Uholanzi, Georginio Wijnaldum aliyetua Paris Saint-Germain (PSG) baada ya mkataba wake ugani Anfield kutamatika mwishoni mwa msimu wa 2020-21.

Shaqiri amewajibishwa na timu ya taifa ya Uswisi mara 96 na alitegemewa sana na kikosi hicho kwenye kampeni za Euro 2020. Alifungia Liverpool mabao manane kutokana na mechi 63. Sita kati ya mechi hizo zilikuwa zile alizosakata katika msimu wake wa kwanza kambini mwa kikosi hicho.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Jifunze kuandaa pankeki tamu za matunda ya blueberries

NASAHA: Ipe mipango yako ya kiakademia kipaumbele ili upate...