• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 6:09 PM
Sharp FC yajitia makali zaidi kuchochea vipaji

Sharp FC yajitia makali zaidi kuchochea vipaji

NA PATRICK KILAVUKA

TIMU ya Sharp FC imejitokeza kuwa moto wa kuotea mbali ikiwa ni kitovu cha kutoa vipaji na kuvilea vyingine katika akademia yake mtaani Eastleigh.

Inajinolea katika uga wa Ziwani, kaunti ndogo ya Starehe, Kaunti ya Nairobi.

Ina wachezaji 32 ambao ni wanafunzi na wengine ni waliomaliza shule.

Chini ya kocha Abdi Nassir, naibu mkufunzi Isa Mohammed, kinara Abdirahaman Ahmed na meneja wa timu Hassan Mustafa, timu hiyo imefaulu kuimarisha talanta na kuwapa vijana fursa ya kujitambua na kukaa mbali na vishawishi vya kutekeleza maovu katika jamii.

Kocha wa Sharp FC Abdi Nassir akiwapa wachezaji mawaidha wakati wa mapumziko katika mchuano wao dhidi ya KSG ugani Kihumbuini. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Aghalabu, lengo la timu ni kuendelea kujisuka kufaa talanta za vijana pamoja na kushiriki Ligi ya Kanda ya Nairobi Mashariki ya Shirikisho la Soka Kenya, ikikwea ngazi ya soka kiligi.

Mwaka wa 2019 ilianza kujituma kwa kujitolea ligi ya Kaunti Ndogo, FKF, Nairobi East na kuibuka kidedea japo ulikuwa mwaka wake wa kwanza.

Kikosi cha Sharp FC (jezi nyeupe) kikicheza dhidi ya KSG uwanjani Kihumbuini PICHA | PATRICK KILAVUKA

Iliweza kufuzu msimu uliofuata katika ligi ya Kaunti, FKF na imeshikilia nafasi ya pili mtawalia kwa misimu miwili 2020-2021na 2021-2022.

Mbali na kufanya vyema katika ligi, katika vipute imedhihirisha ujogoo wao kwa kubeba kombe la Odi Bet mwaka 2021 na 2022 lililoandaliwa jijini Nairobi na Mombasa. Mbali na kunyakua taji la Eastleigh Cup na Green Sport 2021.

Imezalisha vipawa vya soka ambavyo viliangukia majani mabichi katika timu nyingine kama Ahmed Abdullah ambaye ameyoyomea Horseed nchini Somalia, Samuel Saboke na Mickel Kamau ambao wanachezea Rainbow FC.

Kikosi cha KSG FC ambacho kinashiriki ligi ya Daraja la Pili. PICHA | PATRICK KILAVUKA

Chini ya mfadhili Ahmed Gacmey inanuia kushiriki ligi ya Kanda ya FKF, Nairobi East kwa minajili ya kupanua akademia ya soka.

Wameanza  mikakati ya kujinoa zaidi kwa kushiriki katika kipute cha Kangemi Football Association Pre Season ingawa walipigwa katika mchuano wake dhidi ya KSG 1-0

Katika kukiimarisha kikosi wanazamia kusajili wachezaji wengine.

  • Tags

You can share this post!

Matumaini tele kwamba juhudi za Mung’aro zitaimarisha...

Matumaini ya unga wa bei nafuu yafifia

T L