• Nairobi
  • Last Updated May 9th, 2024 3:10 PM
Shujaa yakaribishwa Dubai 7s kwa kichapo kutoka Amerika

Shujaa yakaribishwa Dubai 7s kwa kichapo kutoka Amerika

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Shujaa imeanza duru ya kwanza ya Raga za Dunia za 2021-2022 ya Dubai Sevens vibaya baada ya kuchapwa 14-7 na Amerika nchini Milki za Kiarabu, Ijumaa.

Vijana wa kocha Innocent “Namcos” Simiyu ilizamishwa na miguso kutoka kwa Stephen Tomasin na Logan Tago iliyoandamana na mikwaju yake kutoka kwa Tomasin. Kenya ilifanya makosa kadhaa kwenye skramu zake katika mechi hiyo ya Kundi B yaliyochangia kupigwa kwake.

Kipenzi cha mashabiki Alvin “Buffa” Otieno alishindwa kufanya vitu vyake vinavyofanywa alinganishwe na nyati. Pia, alichangia katika makosa yaliyofanywa kwenye skramu. Shujaa, ambayo ilipata mguso wa kusawazisha 7-7 mapema katika kipindi cha pili kutoka kwa Herman Humwa na mkwaju wa mguso huo kutoka kwa Daniel Taabu, sasa haina ushindi dhidi ya vijana wa kocha Mike Friday katika mechi tatu mfululizo jijini Dubai baada ya kupoteza 26-14 mwaka 2014 na 21-19 mwaka 2017. Mechi mbili za mwisho za Shujaa ni dhidi ya Argentina (1.30pm) na Uhispania (4.02pm).

Makundi ya Dubai 7s I:

Kundi A: Fiji, Australia, Canada, Ufaransa

Kundi B: Argentina, Amerika, Kenya, Uhispania

Kundi C: Great Britain, Afrika Kusini, Ireland, Japan

Matokeo

Afrika Kusini 28 Ireland 7

Great Britain 17 Japan 12

Amerika 14 Kenya 7

Argentina 28-7 Uhispania

You can share this post!

JUMA NAMLOLA: Ni kazi bure kuahidi kuimarisha uchumi bila...

Simbas yakamilisha ziara ya Afrika Kusini kwa kishindo...

T L