• Nairobi
  • Last Updated May 7th, 2024 6:36 PM
Simbas yakamilisha ziara ya Afrika Kusini kwa kishindo ikitupia jicho Uganda

Simbas yakamilisha ziara ya Afrika Kusini kwa kishindo ikitupia jicho Uganda

Na GEOFFREY ANENE

KENYA Simbas inaelekeza macho yake kwa Kombe la Afrika 2022 baada ya kukamilisha ziara yake ya Afrika Kusini kwa kubwaga Diables Barcelona 59-6 Alhamisi usiku.

Simbas, ambayo iliratibiwa kurejea nyumbani jana usiku, ililemea timu hiyo ya Uhispania kupitia miguso ya Derrick Ashihundu (mitatu), John Okoth (miwili), Stephen Sikuta, Elkeans Musonye na Vincent Onyala (mguso mmoja kila mmoja).

Jone Kubu na Matoka Matoka walipachika mikwaju. “Tutachanganua matokeo yetu uwanjani. Tutaangalia tunachohitaji kufanya ili tuzibe mwanya kati yetu na Namibia. Pia, tutamakinikia maandalizi yetu ya mchuano wa robo-fainali ya Kombe la Afrika 2022 dhidi ya Uganda utakaokuwa Julai na kwa mara ya kwanza kutupia jicho Kombe la Dunia 2023 kwa mara ya kwanza tukifuzu,” Odera alieleza Taifa Leo kutoka nchini Afrika Kusini jana.

Alifichua kuwa angependa vijana wake kupata mechi ya kirafiki Aprili baada ya Ligi Kuu nchini (Kenya Cup) kukamilika. Mkurugenzi wa Raga, Thomas Odundo alisema kuwa Simbas imepiga hatua kubwa tangu ziara hiyo ya majuma matatu iliyoshuhudia ikipepetwa 87-15 na Carling Champions na 60-24 dhidi ya Namibia na kuchapa Brazil 36-30.

“Tumeimarika katika ikabu na pia ulinzi,” alisema.

You can share this post!

Shujaa yakaribishwa Dubai 7s kwa kichapo kutoka Amerika

Koome atuliza hofu ya Ruto kuhusu 2022

T L