• Nairobi
  • Last Updated May 18th, 2024 3:46 PM
Sijapata hakikisho mastaa wa Kenya Simbas watashiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia – Odera

Sijapata hakikisho mastaa wa Kenya Simbas watashiriki mechi za kufuzu Kombe la Dunia – Odera

Na GEOFFREY ANENE

KOCHA mkuu wa timu ya taifa ya raga ya wachezaji 15 kila upande, Paul Odera huenda akatumia wachezaji wanaocheza humu nchini pekee kwenye mechi za kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 mwezi ujao.

Amefichua Jumamosi kuwa hajapata hakikisho kuwa ombi lake la kupata ndugu Jeff na Mark Mutuku kutoka Amerika, Andrew Siminyu (Afrika Kusini) na Malcolm Onsando litafaulu. “Habari ambazo napata kutoka kwa Shirikisho la Raga Kenya si kamilifu. Nimeitisha wachezaji hao waletwe kupiga jeki timu, lakini sijapata hakikisho watakuja,” Odera aliambia Taifa Leo.

Timu ya Kenya maarufu kama Simbas, itapepetana na Uganda katika mechi ya kujipima nguvu na pia ya kuwania taji la Elgon Cup mnamo Juni 26.Kisha, Simbas itamenyana na Senegal mnamo Julai 3 na Zambia mnamo Julai 11 katika mechi za raundi ya kwanza ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023.

Mshindi kutoka orodha ya Kenya, Senegal na Zambia ataingia katika raundi ya pili na mwisho kufuzu kushiriki Kombe la Dunia 2023 nchini Ufaransa. Raundi ya pili itafanyika 2022.Aidha, CS Dinamo Bucharest anayochezea Onsando imelipua wenyeji Tomitanii Constanta 71-14 kwenye Ligi Kuu ya Romania, Jumamosi.

Dinamo imetinga miguso 11 na mikwaju minane katika ushindi huo wao wa pili mfululizo baada ya kupiga Chuo Kikuu cha Cluj 35-20 katika mechi iliyopita mnamo Juni 6. Tomitanii imepachika miguso miwili na mikwaju yake.

  • Tags

You can share this post!

Tungali kwenye mataa baada ya kubomolewa makao

Vihiga Queens na Thika Queens walishinda zoni zao za Ligi...