• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 10:15 PM
Sporty FC yajipatia miaka sita itinge Ligi Kuu ya Kenya

Sporty FC yajipatia miaka sita itinge Ligi Kuu ya Kenya

NA JOHN KIMWERE

SPORTY FC ni kati ya vikosi 17 vinavyoshiriki mechi za Kundi B Ligi ya Kanda ya Kati (Central Regional League) kuwania tiketi ya kufuzu kushiriki Ligi ya Taifa Daraja la Pili muhula ujao.

Sporty ya kocha, Margaret Wambui Mwangi inashiriki kipute hicho kwa mara ya kwanza lakini inasadiki kuwa imekaa vizuri kufanya kweli na kubeba tiketi ya kusonga mbele.

”Ninafahamu kuwa endapo tutaendeleza mtindo wa kushinda mechi zetu sio ajabu kutwaa tiketi ya kupandishwa ngazi licha ya kuwa ndio mwanzo tunashiriki ngarambe hii,” kocha huyo alisema na kutoa wito wa wachezaji wake kamwe kutodharau uongozi wa kocha mwanamke.

Anashikilia kuwa wanawake pia wanaweza kuongoza wanaume na kufanya vizuri mradi wajitolee na kujituma kwa udi na uvumba bila kulegeza kamba.

Anahimiza wachezaji wake kushiriki mechi zote kama fainali ili kuhakikisha wanatimiza azma yao ya kufuzu kupandishwa ngazi.

Katika mpango mzima anasema wanahofu wapinzani wao kama SMS Allstars (Tatu City FC) na Kiganjo Kings FC ambao wanaweza kuzima ndoto yao.

Kocha huyo anashikilia wamepania kumaliza kileleni ili kufuzu kushiriki fainali za kuwania tiketi ya kupandishwa ngazi. Kwenye msimamo wa kipute hicho Sporty inafunga tano bora kwa alama 24.

CMS Allstars inaongoza kwa alama 30, tano mbele ya Kiganjo Kings sawa na Gatongora FC tofauti ikiwa idadi ya mabao. Nayo Kiambu Community inashikilia nne bora kwa alama 24.

Anasema akitazama vijana wa kikosi chake hana shaka kutaja kuwa anawapatia miaka sita pekee kuhakikisha wamefanya kweli na kufuzu kushiriki Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka la Kenya (FKF-PL).

Sporty FC ilipopandishwa ngazi ilisajili wachezaji watano wapya ili kuchochea wenzao kwenye kampeni za kipute hicho msimu huu. Ilitwaa huduma za wachana nyavu: Victor Wairimu na Raphael Makumi wote Marafiki FC, Rony Mwangi (Kirinyaga University), Antony Maina (Green Santos) na Francis Muriuki (Githima FC).

Klabu hiii hutugemea huduma za wachezaji mahiri kama mnyakaji Joseph Kang’a, Richard Ngure, Raphael Makumi, Victor Gichohi na Cyrus Wanjohi Kanyoro. Meneja wake, Paulo Kariuki anasema klabu hiyo ikikosa huduma za wachezaji hao itakuwa pigo kubwa kwao.

Imelea

Klabu hii imekuza wachezaji kama Granton Maina (Marafiki FC na Thunder Bird) pia Bob Gathogo (Royal FC).

Klabu hii haina mdhamini ambapo hutegemea michango ya wafuasi wao.

”Bila shaka tunashukuru mashabiki wetu ambao wanazidi kusimama nasi kuhakikisha tunashiriki mechi zetu,” naibu kocha, Duncan Kamau alisema na kuongeza kuwa wanawaombea Mwenyezi Mungu awazidishie ili waendelee kusaidia wachezaji chipukizi kukuza talanta zao.

Mchezaji wa Sporty FC, Joseph ‘Mbariks’ Gikonyo (jezi nyekundu) akishindana na mwenzake wa Kiganjo Kings FC kwenye mechi ya ligi ya kanda ya Kati iliyopigiwa uwanja wa Shule ya Msingi ya Kimunju, Thika. PICHA | JOHN KIMWERE

Sporty FC iliasisiwa mwaka 2017 na hufanyia mazoezi pia huchezea mechi za nyumbani kwenye uwanja wa Tambaya Stadium, Mukurwe-ini Kaunti ya Nyeri.

Sporty inajumuisha: Joseph Kang’a (mlinda lango), Kennedy Wanyiri (naibu nahodha), Richard Ngure, Joseph Gichanga, Marvin Gikonyo, James Weru, Victor Gichohi, Cyrus Wanjohi (nahodha), Raphael Makumi na Josphat Wamwago. Pia wapo: Josphat Mwangi, Joseph Gikonyo, Philip Gakingo, Antony Kamau, Paul Kariira, John Kariuki, John Kibui, Vincent Wahome, Alex Irungu, Antony Maina na Francis Muriuki.

  • Tags

You can share this post!

Wito uchaguzi uwe wa amani Idd-ul-Fitr ikiadhimishwa nchini

Jinsi imani za majini migodini zinavyoleta ufukara Taita

T L