• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
Spurs wazidiwa ujanja katika gozi la Europa Conference League

Spurs wazidiwa ujanja katika gozi la Europa Conference League

Na MASHIRIKA

TOTTENHAM Hotspur walilipia maamuzi ya kuacha nje wachezaji wao wa haiba kubwa wakati wa mechi ya Europa Conference League iliyowakutanisha na Vitesse Arnhem ya Uholanzi mnamo Alhamisi usiku.

Vitesse walifunga bao la pekee na la ushindi katika mechi hiyo kupitia penalti ya Maximilian Wittek katika dakika ya 78. Ushindi huo wa Vitesse ulining’iniza pembamba matumaini ya Spurs ya kocha Nuno Espirito kusonga mbele kwenye kipute hicho kutoka Kundi G.

Baada ya kupumzisha wanasoka wa haiba kubwa kama vile Harry Kane na Son Heung-min, Spurs walipanga kikosi dhaifu zaidi dhidi ya Vitesse huku wakifanyia mabadiliko tisa kikosi kilichopiga Newcastle United katika mechi ya awali ya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL).

Vitesse waliokamilisha kampeni za Ligi Kuu ya Uholanzi (Eredivisie) mnamo 2020-21, walipata nafasi nyingi za kufunga mabao ila wakazipoteza.

Kichapo kwa Spurs kiliwasaza katika nafasi ya tatu kwenye Kundi G baada ya kuambulia sare dhidi ya Rennes ya Ufaransa na kupepetwa na Mura ya Slovenia katika mechi mbili za ufunguzi.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Mourinho apokezwa kichapo kinono zaidi katika historia yake...

WASONGA: Serikali ifute mikataba ghali ya ununuzi stima

T L