• Nairobi
  • Last Updated May 12th, 2024 5:17 PM
Three Lions wanoma!

Three Lions wanoma!

Na MASHIRIKA

LONDON, Uingereza

KUFUATIA ushindi mnono wa 10-0 dhidi ya San Marino katika pambano la kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022, Uingereza imesawazisha rekodi yake ya ufungaji mabao katika mechi ya ushindani.

Katika mchuano huo ambao nahodha Harry Kane alifunga mabao manne, kikosi cha Gareth Southgate maarufu kama Three Lions – ambacho sasa kimefuzu kwa dimba hilo nchini Qatar – kilivuruga ngome ya San Marino bila huruma.

Mabao mengine yalipatikana kupitia kwa Emile Smith Rowe, Bukayo Saka, Tyrone Mings, Harry Maguire na Tammy Ibrahim.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa Uingereza kufunga mabao 10-0 tangu Mei 1964 ilipoicharaza Amerika 10-0, lakini haikufanikiwa kuvunja rekodi yake ya 13-0 dhidi ya Ireland iliyoweka mwaka 1882.

Uingereza wamemaliza katika nafasi ya kwanza katika Kundi A kwa pointi 26 baada ya Poland kushindwa na Hungary 2-1 katika mechi nyingine yakundi hilo.

Tayari Poland walikuwa wamefuzu kwa mchujo wa kuwania nafasi ya kufuzu baada ya ushindi wa awali wa 4-1 dhidi ya Andora kwenye mechi iliyochezwa Ijumaa.

Hungary ilijipatia bao la kwanza dakika ya 37 kupitia kwa Andras Schafer kabla ya Karol Swiderski kusaawzisha dakika ya 61.

Bao la ushindi la Hungary lilifungwa na Daniel Gazdag dakika ya 80 baada ya kupenya ngome ya Poland kabla ya kumchanganya kipa Wojciech Szczesny.

Kwingineko, mashabiki wa timu ya taifa ya Ufaransa wanaendelea kumshambuliaji Matteo Guendouzi kufuatia maoni yake kwamba alitaka mechi yao na Kazakhstan ichezewe uga wa Stade de France badala ya Parc des Princes, mwishoni mwa wiki.

Ilikuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo wa Arsenal anayechezea Marseille kwa mkopo kujumuishwa kikosini tangu miaka miwili iliyopita.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 hajawahi kuchezea timu kuu lakini aliitwa kujiunga na kikosi hicho mwezi Septemba.

Katika mechi za kufuzu za bara Afrika, Togo na Niger zilimaliza mechi zao za mchujo wa kufuzu kwa Qatar 2022 kwa ushindi Jumatatu lakini ushindi huo haujaziwezesha kusonga mbele.

Togo waliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Namibia kutokana na bao la Meme Placca, akini uishindo haukuwasaidia. Peter Shalulile wa Namibia alishindwa kufunga penalti baada ya kipa Wassiou Ouro-Gneni kuzuia mkwaju wake.

Niger ilimaliza mechi zake za Kundi A kwa ushindi mkubwa wa 7-2 dhidi ya Djibouti.

Victoria Adebayor alifunga matatu huku mengine yakipatikana kupitia kwa Amadou Wonkoye (2), Daniel Sosah na Youssouf Ahmed.

Katika mechi nyingine, guinea-Bissau na Sudana zilitoshana nguvu kwa kutofungana katika Kundi A.

Morocco, ambao tayari wamefuzu kutoka kundi hilo, walitarajiwa kualika Guinea jana Jumanne.

  • Tags

You can share this post!

Utafunaji miraa unaharibu hali ya usafi – Jaji

Kananu achukua usukani kama gavana Nairobi

T L