• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 10:48 AM
Utafunaji miraa unaharibu hali ya usafi – Jaji

Utafunaji miraa unaharibu hali ya usafi – Jaji

Na MAUREEN ONGALA

JAJI wa Mahakama ya Malindi, Bw Stephene Githinji, amelaumu uraibu wa utafunaji miraa na muguka kwa uchafuzi wa mazingira.

“Kiwango kubwa ya uchafu ni karatasi za peremende za kutafunia miraa na mugokaa. Inadhihirisha kuwa watu wengi hutafuna na kutupa taka kila sehemu,” akasema akishirikiana na wakazi kusafisha mji wa Malindi.

Takriban kilo 168 za taka ziliokotwa katika shughuli hiyo iliyohudhuriwa pia na mkuu wa kampuni ya Jambojet, Bw Karanja Ndegwa.

Bw Ndegwa aliwahimiza wananchi kudumisha usafi kila mara na kusema shirika hilo la ndege litaendelea kusaidia katika usafishaji wa mji wa Malindi.

Mpango wa kusafisha Malindi husimamiwa na kikundi cha Progressive Welfare Association Malindi (PWAM) kupitia kwa mfumo wa nyumba kumi.

Mpango huo unajumuisha zaidi ya wadau 40 kutoka sekta mbalimbali wakiwemo waekezaji wa hoteli, wafanyabiashara katika fuo za bahari, idara ya usalama na wakazi.

You can share this post!

CECIL ODONGO: Msimamo mkali wa Mudavadi huenda ukamsukuma...

Three Lions wanoma!

T L