• Nairobi
  • Last Updated April 28th, 2024 4:55 PM
Timu ya Zetech Rugby yaonyesha ubingwa wake

Timu ya Zetech Rugby yaonyesha ubingwa wake

Na LAWRENCE ONGARO

TIMU ya Rugby ya Zetech Oaks imeonyesha ubingwa wake na kuibuka washindi katika eneo la kati.

Kocha wa timu hiyo Rumsfeld Matakwa, anasema kuwa amekuwa na kikosi hicho kwa miaka minne mfululizo huku akiweka klabu ya Zetech katika ramani ya michezo kote nchini. Kocha huyo anakipongeza chuo cha Zetech kwa kuweka vijana hao katika nafasi njema kimichezo Jambo ambalo limewapa motisha ya kujizatiti zaidi.

Anawapongeza maafisa wakuu wa klabu hiyo kwa kuwa mstari wa mbele kuhakikisha wanapata kila msaada wanaostahili kupata. Aliwataja kama Wycliff Sirengo, anayesimamia michezo za chuo hicho. Mwingine ni meneja wa klabu ambaye ni Nickson Muturi ambaye amekuwa mstari wa mbele kuona ya kwamba kila mchezaji anapata mahitaji muhimu ya michezo.

Kocha huyo alisema ananoa kikosi cha wachezaji 25 ambao ndio wameipa klabu hiyo uhai. Baadhi ya wachezaji wanaoipa klabu ya Zetech uhai ni Jeremy Lwande, Eugen Odhiambo, Mike Wekesa ,Dihary Hope na Felix Ouma. Wengine ni Bryan Chemuku Augustine Simiyu na Jack Mangale pia kuna Fidel Joshua Johnson Wafula Collins Ochieng’ Boaz Wafula na Jared Obuya.

Kulingana na kocha huyo anasema kuwa hivi majuzi timu hiyo iliongoza Ligi ya Rugby ya eneo la kati kwa kuzoa jumla ya pointi 39. Anaeleza Jambo ambalo limefanya kuweka timu hiyo mbele ni vijana wake kudumisha nidhamu na kuhudhuria mazoezi kila mara bila kuchelewa. Kocha huyo ametoa hakikisho kuwa vijana wake wataendelea kutamba katika mchezo huo kwa sababu wamejitolea mhanga kuona ya kwamba wanafanikiwa.

Anasema kile kinachowapa motisha ya kuendelea kuongoza ni kila mchezaji anaonyesha kipaji chake akiwa uwanjani na kila mmoja huonyesha staili tofauti ya kukabiliana na mpinzani wake. Anasema lengo lake kuu ni kuona ya kwamba klabu ya Rugby ya Zetech inatambulika kote nchini na kushiriki Ligi ya Kitaifa.

Anaeleza kuwa ili mchezaji kufanikiwa katika mchezo huo ni sharti mchezaji ajitolee mhanga Kwa kufanya mazoezi kwa bidii kwa sababu mchezo huo inahitaji mchezaji kutumia nguvu nyingi.

You can share this post!

Biashara ya siagi yafaidi walemavu

Wafanyakazi wa kampuni ya KPLC washtakiwa kwa wizi

T L