• Nairobi
  • Last Updated May 2nd, 2024 8:55 PM
TUSIJE TUKASAHAU: Ni muhimu walimu wakuu watafute idhini ya wizara kabla mabasi kutumika kwa shughuli za kijamii

TUSIJE TUKASAHAU: Ni muhimu walimu wakuu watafute idhini ya wizara kabla mabasi kutumika kwa shughuli za kijamii

WATU wawili walifariki jana katika ajali iliyohusisha Basi la Shule ya Upili ya Wasichana la Moi Suba katika soko la Ekerenyo, kaunti ya Nyamira mnamo Jumatano wiki hii.

Basi hilo lilikuwa likisafirisha waumini wa Kanisa la Repentance Holliness Ministry kutoka Migori kuelekea Nakuru kwa shughuli za kidini.

Japo, mabasi ya shule bado yanakodishwa kwa matumizi ya shughuli zisizo za kimasomo, walimu wakuu wasije wakasahau kwamba mnamo Juni 15, 2021, aliyekuwa Waziri wa Elimu George Magoha alipiga marufuku mwenendo huo.

Akiongea katika Taasisi ya Kuunda Mtaala Nchini (KICD) alipokuwa akizindua shughuli ya uteuzi wa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza, Profesa Magoha alisema walimu wakuu sharti wapate idhini kutoka kwa makao makuu ya Wizara ya Elimu, Nairobi.

Mara nyingi mabasi ya shule hukodishwa na watu wanaoenda katika shughuli za kijamii kama vile, mazishi, harusi na hafla za makundi ya akina mama na vijana.

Ni nyakati za shughuli kama hizi ambapo basi hizi huhusika katika ajali na kusababisha maafa.

  • Tags

You can share this post!

Mshukiwa wa utapeli Mulot anaswa na polisi

DOUGLAS MUTUA: Kwaheri 2022, mwaka uliokuwa ‘mrefu...

T L