• Nairobi
  • Last Updated May 17th, 2024 11:53 AM
DOUGLAS MUTUA: Kwaheri 2022, mwaka uliokuwa ‘mrefu zaidi’ kuliko kawaida

DOUGLAS MUTUA: Kwaheri 2022, mwaka uliokuwa ‘mrefu zaidi’ kuliko kawaida

NA DOUGLAS MUTUA

MWAKA 2022 unaisha leo! Labda ni kwangu mimi, lakini nahisi kama mwaka huu umekuwa mrefu kuliko mingine yoyote.

Bila shaka una siku 365, lakini zimeonekana kujikokota sana hivi kwamba nahisi kama zimekuwa maradufu.

Tuliusubiri mwaka wenyewe kwa miaka minne na ushei! Kisan a maana Uchaguzi Mkuu, hasa wa urais, ambao ulifanyika mwezi Agosti.

Labda kwa kuusubiri sana kwa sababu za kisiasa, siku ya siku ikafika kisha tukafanya uchaguzi na maisha kuendelea kama kawaida, ndio maana nahisi kama umekuwa mrefu.

Labda mwaka huu ulipaswa kuisha baada ya Uchaguzi Mkuu, tuanze mwaka mpya, serikali mpya, rais mpya na maisha mapya.

Pengine tunapaswa kubadilisha sheria ili Uchaguzi Mkuu uwe ukifanyika wiki ya mwisho wa mwaka, yaani baada ya Sikukuu ya Krismasi na kabla ya ile ya Mwaka Mpya.

Hizo ni siku ambazo Wakenya hupoteza bure wakirandaranda mashambani baada ya kusherehekea Krismasi kwa kuwa hawataki kurejea mijini na kuanza kazi.

Tunapofanya uchaguzi mkuu mwezi Agosti tunavuruga ratiba za masomo, kazi na maisha ya watu kwa jumla, yakitulia kidogo sikukuu inafika na mbio zake za kwenda mashambani.

Uchaguzi ukifanyika Disemba, kila kitu kitakuwa kipya mwaka utakaofuata; Mahakama ya Upeo itashughulikia kesi mpya ya uchaguzi iwapo mshinde akikataa matokeo.

Hata Bunge litakuwa jipya, sura nyinyi mpya-mpya, kwa sababu kawaida ya wabunge, asilimia 75 huishia kuyaona paa majengo ya Bunge kwa kuwa hawachaguliwi tena.

Nadhani sababu nyingine ya kuhisi kwamba mwaka huu umekuwa mrefu zaidi ni kuchoshwa na mihemko ya kisiasa ambayo ilitawala kipindi kizima cha miezi 12.

Watu walitukanana kwenye mikutano ya hadhara na mtandaoni, marafiki wakawa maadui, watu wakalizana machozi kwa unoko wa kupigiwa mfano.

Na kwa kuwa kawaida ya binadamu hakuumbwa kuishi na hamaki kiasi hicho, anatamani mwaka huu uishe ausahau, maisha yake yarejee katika hali ya kawaida.

Binafsi natamani uhasama na chuki viishe kati ya waliounga mkono makundi mbalimbali katika uchaguzi huo ili tuungane kuikosoa serikali kwa sauti moja kila inapofanya makosa.

Tangu uchaguzi uishe, hali imekuwa kwamba walioichagua serikali ya sasa wanawaona wasioichagua kama maadui zao badala ya washirika katika kuiwajibisha.

Nao wasioichagua wanaomba ishindwe katika makjukumu yake, sikwambii tayari wameanza kuicheka na kushangilia ‘mateso’ ya walioichagua.

Maneno kama ‘tutateseka pamoja’ yamekuwepo kwa muda sasa, hasa kutoka kwenye vinywa vya waliojaribisha bahati wakashindwa, mtazamo amboa unapaswa kubadilishwa.

Samahani, lakini nadhani unaposherehekea kwamba serikali imeshindwa kukuhudumia, unayacheka masaibu yako mwenyewe, hivyo ni sahihi kusema unatumia akili kama kofia.

  • Tags

You can share this post!

TUSIJE TUKASAHAU: Ni muhimu walimu wakuu watafute idhini ya...

WANDERI KAMAU: Tukome kumlaumu shetani kwa kutojali na...

T L