• Nairobi
  • Last Updated May 19th, 2024 6:50 AM
Uefa yaadhibu vikali vikosi tisa kati ya 12 vilivyoasisi kipute kipya cha European Super League

Uefa yaadhibu vikali vikosi tisa kati ya 12 vilivyoasisi kipute kipya cha European Super League

Na MASHIRIKA

VIKOSI tisa kati ya 12 vilivyokuwa vya kwanza kuingia katika mpango wa kuasisi kipute kipya cha European Super League (ESL) vimeadhibiwa na Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa).

Klabu hizo ni pamoja na Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City, Manchester United, Tottenham Hotspur, AC Milan, Inter Milan na Atletico Madrid.

Kwa mujibu wa Aleksander Ceferin ambaye ni rais wa Uefa; klabu za Real Madrid, Barcelona na Juventus zitapokezwa adhabu kali zaidi baada ya kukamilika kwa mchakato wa nidhamu utakaosimamiwa na kamati kuu tendaji ya Uefa.

Kufikia sasa, Real, Atletico na Juventus ndivyo vikosi vitatu vya pekee ambavyo havijatangaza kujiondoa kwenye gozi la ESL lililotangazwa mnamo Aprili 18. Klabu sita kuu za Ligi Kuu ya Uingereza (EPL) zilijitoa kwenye kivumbi hicho saa 48 baadaye kwa sababu ya hisia mseto zilizoibuliwa na mashabiki na wadau wa soka duniani.

Kila mojawapo ya klabu hizo tisa zilizoadhibiwa na Uefa zinastahili sasa kutoa kima cha Sh1.8 bilioni ambazo zitasambazwa kwa watoto kutoka familia zisizojiweza na akademia za wanasoka chipukizi kutoka timu za mashinani barani Ulaya.

Aidha, kila klabu itashuhudia asilimia tano ya mapato kutokana na ushiriki wa mechi za bara Ulaya ikiondolewa na Uefa kuanzia msimu wa 2023-24. Fedha hizo zitatengewa maendeleo ya soka ya mashinani katika mataifa mbalimbali ya bara Ulaya.

Manchester United wamefichua kwamba faini hiyo italipwa na mmojawapo wa wenyeviti wao, Joel Glazer, kutokana na mapato ya biashara zake binafsi kwa sababu kikosi hakitagharimika kwa vyovyote vile.

Hali sawa na hiyo itashuhudiwa kambini mwa Arsenal ikizingatiwa kwamba wamiliki wa kikosi hicho, Kroenke Sports and Entertainment, wamesisitiza kwamba watasimamia gharama hiyo wao wenyewe.

Mbali na kutozwa Sh1.8 na asilimia tano ya mapatano ya kushiriki vipute vya UEFA na Europa League kuondolewa kuanzia 2023-24, kila mojawapo ya klabu tisa kati ya 12 zilizohusishwa kwenye uasisi wa ESL zimepigwa faini ya Sh12 bilioni.

  • Tags

You can share this post!

Ajax na Man-United katika vita vya kumsajili fowadi mahiri...

COVID-19: Mashabiki wa Chelsea na Man-City kukosa...