• Nairobi
  • Last Updated May 6th, 2024 4:43 PM
COVID-19: Mashabiki wa Chelsea na Man-City kukosa kuhudhuria fainali ya UEFA nchini Uturuki

COVID-19: Mashabiki wa Chelsea na Man-City kukosa kuhudhuria fainali ya UEFA nchini Uturuki

Na MASHIRIKA

MASHABIKI wa Chelsea na Manchester United wameshauriwa kutosafiri nchini Uturuki kuhudhuria fainali ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) itakayokutanisha vikosi hivyo jijini Istanbul mnamo Mei 29, 2021.

Hii ni baada ya serikali ya Uingereza kutia Uturuki kwenye orodha ya mataifa yanayoshuhudia maambukizi zaidi ya virusi vya corona.

Katibu wa Uchukuzi, Grant Shapps, amesema kwamba mataifa yote yaliyo kwenye orodha yao ‘hatari’ hayasatahili kutembelewa na wakazi na raia wa Uingereza isipokuwa katika hali ambazo “zinalazimu ziara hizo kuandaliwa”.

Aidha, amependekezea Shirikisho la Soka la bara Ulaya (Uefa) kuruhusu kivumbi hicho kuandaliwa uwanjani Wembley, Uingereza.

Yalikuwa matarajio ya vinara wa Uefa kuwapa angalau mashabiki 4,000 kutoka kila kikosi tiketi za kuhudhuria fainali hiyo ya Klabu Bingwa uwanjani Ataturk Olympic.

Kwa mujibu wa Schapps, Shirikisho la Soka la Uingereza (FA) linajadiliana na Uefa kuhusu uwezekano wa kuhamishia gozi hilo hadi ugani Wembley kwa sababu ya urahisi wa kuliandaa ikiwangatiwa kwamba wanafainali wote wawili wanatokea Uingereza na uwanja wa Wembley si nyumbani kwa yeyote kati ya Chelsea na Man-City.

Wakazi na raia wa Uingereza wanaorejea nchini humo kutoka mataifa yaliyo kwenye orodha yao ya hatari wanahitajika kujitenga kwa siku 10 katika hoteli ambazo zimeidhinishwa na serikali.

Hatua hiyo itaathiri pakubwa maandalizi ya baadhi ya wachezaji wa Chelsea na Man-City watakaohusika moja kwa moja katika fainali za Euro 2021 zitakazoanza Juni 11 hadi Julai 11, 2021. Michuano mingi ya Euro itaandaliwa katika uwanja wa Wembley, Uingereza.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

  • Tags

You can share this post!

Uefa yaadhibu vikali vikosi tisa kati ya 12 vilivyoasisi...

China yahimiza huduma bora za kulinda watoto wakitoka...