• Nairobi
  • Last Updated May 4th, 2024 7:55 AM
Uhitaji wa jezi ya Ronaldo waongezeka kwa asilimia 3,000

Uhitaji wa jezi ya Ronaldo waongezeka kwa asilimia 3,000

Na MASHIRIKA

UHITAJI wa jezi nambari saba mgongoni inayovaliwa na supastaa Cristiano Ronaldo katika kikosi cha Manchester United umeongezeka kwa zaidi ya asilimia 3,000 tangu nyota huyo raia wa Ureno abanduke Juventus nchini Italia na kurejea ugani Old Trafford.

Uhitaji wa jezi hiyo umeongezeka baada ya Ronaldo kufunga mabao matano kutokana na mechi tano zilizopita ambazo ametandazia Man-United ya kocha Ole Gunnar Solskjaer katika mashindano yote ya hadi kufikia sasa muhula huu.

Ingawa Ronaldo hutia mfukoni mshahara wa Sh74.8 milioni kwa wiki kambini mwa Man-United, kikosi hicho kimepania kurejesha asilimia kubwa ya gharama hiyo ya matumizi ya fedha kutokana na mauzo ya jezi ya nyota huyo wa zamani wa Real Madrid.

Kwa mujibu wa jarida la 888 Sport nchini Uingereza, uhitaji wa jezi ya Ronaldo ulifikia asilimia 3,000 usiku wa Jumatano baada ya sogora huyo kufungia Man-United bao la ushindi katika sekunde za mwisho za mchuano wa Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) dhidi ya Villarreal ugani Old Trafford.

Baada ya kipenga cha kuashiria mwisho wa mechi hiyo kupulizwa, idadi ya mashabiki walioagiza jezi ya Ronaldo ilifikia asilimia 3,173 huku asilimia 408 ya jezi zote zilizoagizwa zikiuzwa usiku huo.

The average cost of a Man Utd replica shirt is £64.95 with a ‘Ronaldo 7’ costing £79.95.An authentic match quality version sets punters back £120.Bei ya jezi moja ya inayovaliwa na Ronaldo kambini mwa Man-United ni Sh12,470 huku mfano wa jezi hiyo ikinadiwa kwa Sh10,130.

Ingawa jezi ya Man-United ni ghali, haiko miongoni mwa jezi 10 ghali zaidi katika soka ya bara Ulaya.Jezi ya Nike ya Barcelona ndiyo ghali zaidi barani Ulaya na inauzwa kwa Sh12,735 sawa na bei ya jezi ya Cagliari inayoshiriki Ligi Kuu ya Italia (Serie A).

Jezi ya kampuni ya Kappa inayovaliwa na wanasoka wa Fiorentina ya Serie A ndiyo ya bei ya chini zaidi katika soka ya bara Ulaya na inauzwa kwa Sh5,220.Miongoni mwa vikosi vya Ligi Kuu ya Uingereza (EPL), vikosi vyenye jezi nafuu zaidi ni Burnley (Sh7,020), Brentford (Sh7,488), Crystal Palace (Sh7,800) na Norwich City (Sh7,800).

Jezi ghali zaidi katika soka ya EPL ni za vikosi vya Tottenham Hotspur (Sh10,920), Chelsea (Sh10,900) na Liverpool (Sh10,900).

  • Tags

You can share this post!

Vipusa wa Man-City na Chelsea kukutana kwenye nusu-fainali...

Google kufuta jumbe potovu kuhusu chanjo ya corona YouTube